Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielezea kuhusu hisia za kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).   Waziri Membe alikuwa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akiendelea na mahojiano hayo, wakati Bi. Fauzia Yusuph wa Channel Ten akirekodi tukio hilo. 

Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameelezea hisia za sintofahamu kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhoji kuwa iwaje nchi yetu itengwe na nini maana ya Jumuiya hiyo?
Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.  Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kujua msimamo wa Tanzania kidiplomasia wakati huu wa sintofahamu ya Jumuiya hiyo inayoendelea, hususan Tanzania ikionekana kutengwa na nchi za Uganda, Rwanda na Kenya.
“Huu ni muungano wa watu wenye woga,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika mnamo mwaka 1977.  
“Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika.  Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe.  Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.
“Sisi ndio ‘center of gravity’ na ndio soko kubwa la bidhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki - tuna rasilimali zaidi ya majirani zetu, tuna utajiri wa ardhi na bandari nne ambazo ni ufunguo wa kutumia bahari kubwa na kufikia nchi nyingine duniani,” alifafanua Waziri Membe.  Bandari hizo ni za Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na bandari ya Bagamoyo ambayo ipo katika ujenzi wa kuifanya iwe bandari kubwa ya kimataifa barani Afrika.
Waziri Membe alisema cha kushangaza ni kwamba majirani zetu wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ambayo ni mfano pekee wa kuigwa kwa uzoefu wa muungano.  “Sisi ni taifa na sio muungano wa makabila matatu au manne,” alisema Waziri huyo.
“Hauwezi leo ukaitaifisha ardhi ya nchi nyingine na kuviacha vizazi vijavyo bila mali,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa “kwa vyovyote vile, jumuiya hii ya Afrika Mashariki lazima iende kwa taratibu.”
Aidha, Waziri Membe alienda mbali zaidi na kusema kuwa huenda chokochoko ya kutengwa kwetu inatokana na wivu au gere kwa Tanzania kupeleka majeshi yake huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo alilosema huenda halijawafurahisha baadhi ya watu katika Jumuiya hiyo.
Vilevile alisema kuwa kitendo cha Tanzania kukataa ardhi kuwa sehemu ya mali ya Afrika Mashariki huenda pia imepelekea mchango mkubwa kwenye choko choko hizo.
Waziri Membe amewaambia Watanzania kuwa “wakae wakijua kwamba akufuzae hakwambii toka, utaona tumambo yanabadilika.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Well said Mh. Membe, ni bora tujitenge kuliko kuwa na hawa jamaa. Tuimarishe tu jeshi letu maana hawakawii kuleta chokochoko.

    ReplyDelete
  2. Tunataka viongozi wenye misimamo kama hivi. Hakuna kuyumba. Endelea na uzi huo huo tutakufikiria 2015 au 2020!

    ReplyDelete
  3. ARDHI ni ajira wazalendo na ibaki mikononi mwetu. Tuwaache waendelee na sisi tuendelee na yetu. Tusiwabembeleze.

    ReplyDelete
  4. Mhe.Membe.

    Sisi Tanzania ndio watoaji Talaka, na sio wao.

    -Tuna 52% ya eneo la EAC.
    -Tuna Rasilimali nyingi na Utajiri zaidi yao.
    -Tuna Majirani mbadala (Congo-DRC US$ 24 Tri. & Angola US$ 13Tri., Msumbiji Gas-LNG 200 TCF na Mauritius) wenye tija kuliko wao majirani wao mbadala WAPO HO (South Sudan, Ethiopia na Somalia) wakivunja Umoja na sisi watapoteza zaidi.

    Hivyo sisi ndio WAUME ktk hii EAC na hivyo kwa utamaduni wetu Tanzania ndio watoaji wa Talaka na kwa msingi huo hapo juu ni wazi ndio tutafungua njia kumpata MKE MWEMA NA MWENYE KUTOKA UKOO TAJIRI ZAIDI NA WA DARJA LA JUU KULIKO MKE WA SASA WA EAC YA UKOO WA MASHAKA MASHAKA!!!

    ReplyDelete
  5. Ardhi ni mali ya taifa sio mataifa. Uhusiano wa EAC usiwe na ulafi wa nchi kutaka kuvutia wengine wote upande mmoja dhidi ya nchi nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...