Naibu Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dr. Abby Nangawe akiongea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuo hicho.Katika ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara huo na kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE Godian Bwemelo.Mhadhara huo ulifanyika jana chuoni hapo jijini Dra es salaam.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akizungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo wa wazi chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta ya masoko na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akionesha kwa vitendo mbinu za kimasoko Wakati alipoalikwa kuzungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa ni mmoja kati ya vijana waliobobea katika Nyanja ya masoko na matangazo nchini na alialikwa chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta hizo na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(hayupo pichani) ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuoni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...