
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba kitafanya uzinduzi wa album yake nzuri sana ya "Yesu ni Mwema", na utambulisho wa album nyingine kama “Nakushukuru Mungu”, “Zawadi ya Krismasi" n.k siku ya Jumapili tar. 10/11/2013 katika ukumbi wa Triple A - Arusha.
Kiingilio kitakuwa 10,000 kwa mtu mmoja (single size ticket) na 50,000 kwa watu 6 (Family size ticket). 
KAPOTIVE Star Singers-Bukoba wamejizolea umaarufu katika uimbaji mahiri, na maonesho yao makubwa ambayo yamefanyika Bukoba na Dar-es-Salaam na Mwanza yaliwavutia wengi.
Watu wa Arusha msikose burudani ya aina yake siku ya Jumapili tar. 10/11/13 katika ukumbi wa Triple A, katikati ya jiji la Arusha. Karibu tuwaunge mkono vijana wetu.
Baadhi ya wachezaji wa Kwaya ya Kapotive Star Singers - Bukoba wakiimba nyimbo zao kwenye matamasha yao


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...