Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya akimkabidhi cheti maalum mmoja kati ya viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari nchini, vyeti ambavyo vinatolewa kwa wanachama wa vilabu ambao wamepatiwa mafunzo mbali mbali.
Na Francis Godwin, Mwanza
UMOJA wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanza utaratibu wa kutoa vyeti maalum kwa wanachama wa klabu za waandishi wa habari nchini ambao wanapatiwa mafunzo mbali mbali.
Mkurugenzi mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan alisema kuwa vyeti hivyo vimeanza kutolewa baada ya maadhimio ya wajumbe wa mkutano mkuu.
Hivyo alisema kuanzia sasa wanachama wa vilabu ambao watapewa mafunzo wanachama wake watapewa vye vyeti maalum .
Pia alisema vyeti hivyo vitakuwa vya viwango vya juu na vinaanza kutolewa sasa kwa vilabu hivyo.
Wakati huo huo umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umewataka viongozi wa vilabu hivyo mikoani kutumia changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao kujipanga badala ya kuzichukia changamoto hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza na Rais wa UTPC Kenneth Simbaya wakati akifungua mkutano mkuu wa wanachama wa klabu za waandishi wa habari.
Simbaya alisema kuwa mbali ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika klabu vya waandishi wa habari nchini ila bado wapo baadhi ya viongozi ambao wameendelea kukwepa changamoto mbali mbali badala ya kuzifanyia kazi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...