Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimtambulisha Mhe. Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa pamoja na Waandishi hao kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa hivi karibuni kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika hotuba hiyo Mhe. Rais Kikwete alieleza msimamo wa Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mhe. Amina Mohammed akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huku Mhe. Membe akisikiliza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John haule (wa pili kulia) akimsikiliza Mhe. Mohammed (hayupo pichani) alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana (wa pili kushoto) na Mjumbe kutoka Kenya.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Robert Kahendaguza (kushoto), Mjumbe kutoka Kenya na Bw. Mkumbwa Ally (mwenye koti jeusi), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Membe na Mhe. Mohammed na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. They just want to use Tanzania to help Uhuru with his case at ICC.

    ReplyDelete
  2. Tahadhali kwa serikali yangu ya Tanzania na kwa watanzania,,ndugu zanguni tuwe makini sn na hawa watu coz ni mandumila kuwili,,nn chakufanya Misimamo yetu na sera zetu kama vile ARDHI, AJIRA ZETU,mambo ya UHAMIAJI,yasiwe kabisa katika hii Jumuiya,,ni hayo tu kwaleo ijapokua nina mengi ya kuongelea kuhusu hao majirani wanafiki,,mm huku UINGEREZA niliko napambana nao ile mbaya kuanzia wanyarwanda,waganda,mikenya,hasa hasa kwenye mambo ya ARDHI na AJIRA,mm nawaambia ya kwamba nyie kwenye nchi zenu bado mnasera za kikoloni but TZ tuko out of hizo sera zenu,ndio maana kwetu amani tele na upendo tele,basi yatanuna weee na mm nawaambia mtanuna sn na sn,naitwa mdudu kakakuona,

    ReplyDelete
  3. uncle p/se post this
    thanks;
    Mambo ya kuwa kimbele-mbele
    katika kesi ya Uhuru ICC na yaishe.
    Mara tumeandika barua ICC/UN kumuombea msamaha.
    Yeye mwenyewe alisema kesi yake na ICC ni suala la kibnafsi. Sasa sisi kinatukera kitugani,mpaka mwanasheria wetu mkuu aliandika barua ya kumuombea msamaha.
    Vile usisahau kuwa hao mashahidi waliompeleka huko ICC ni wakenya wenzake,kama yeye yuko safi basi wangemalizana wenyewe kwa wenyewe.
    Ni hao hao Wakenye wenyewe kwa maksudi walimchagua Uhuru tayari akiwa ni Mtuhumiwa mwenye kesi ya mauaji iliyokuwa ikindelea.Sasa kwa unafki wanajifnya wanashangaa Mtuhumiwa Rais wao atasimamishwa kizimbani.
    Tusikubali watutumie kama vile sisi ni Wizara Fulani katika serikali yao.

    ReplyDelete
  4. Wakenya asante kwa Pongezi zenu kwetu.

    Mambo ya Muhimu ni haya:

    1.Tupo katika Muungano wa EAC na nyinyi ndugu zetu, hivyo na sisi tunahitaji kutetea Maslahi yetu ktk Muungano na kuwa hatuwezi kusaini kila Azimio lililopo mezani lazima tunagalie na sisi upande wetu mfano masuala hayo ya ARDHI, AJIRA na UHAMIAJI aliyosema Raisi wetu.

    Mfano ktk Umoja wa Ulaya, nchi zingine zinatumia Sarafu yao mfano Uingereza, Uswisi na Norway.

    Hivyo Maamuzi ya kusaini Maazimio ktk Muungano wetu yawe kwa ridha na sio kwa kulazimishana na kushinikizana kusaini...kuwa ktk Muungano wa EAC sio kuwa ''Mr. Yes'' kwa kila azimio linalowekwa mezani.

    2.Jihadharini sana na Mwanacha wa mpya wa Jumiuya Rwanda aliye kubaliwa mwaka 2010, kwa miaka mitatu (3) tu aliyokuwepo ndani ya Jumuiya joto ya jiwe tumeiona ndio haya ya 'Coalition of willing' inaonekana amekuja na hulka mbaya ya kulazimisha mambo na kuleta utengano ndani ya Jumuiya.

    Ninyi Kenya ni ndugu zetu wa karibu sana kwa mengi, angalieni ktk Jumuiya ya mwanzo iliyo vunjika mwaka 1977 wote tulikuwepo wakati Rwanda haikuwemo.

    3.Sote kwa pamoja Kenya na Tanzania tuangalie changamoto zilizopo mbele yetu NA KUZITATUA KWA MAENDELEO YETU badala ya kuchochea utengano kwa vile KIVITENDO (PRACTICALLY) TANZANIA HAIWEZI KUTENGANA NA KENYA!!!


    MWELEZENI WAZI KAGAME AACHE MIPANGO YAKE YA UTENGANO ''Coalition of willing'' ALIYO ASISI YEYE NA KTIBU MKUU WA EAC Dr.SEZIBERA.

    ReplyDelete
  5. watanzania wenzangu kawa wewe ni mchapa kazi na mwadilifu basi huna haja ya kuogopa ajira maana waajiri wengi Tanzania wanakutafuta, kama ni mvivu, domo kaya, basi si shaka lazi ma uogope maana hutapata kazi. Waajiri wengi wamewekwa mateka na wafanyakazi wao wavivu na bila shaka wakipata ruhusa ya kuajiri hata nje ya tanzania basi wanafurahi sana. Tuchape kazina tusiogope, alexbura dar

    ReplyDelete
  6. Raisi Kikwete alihutubia Afrika ya Mashariki nzima !

    Hotuba ilikuwa imekwenda shule na yenye akili,

    1.KENYA,
    Jana kwa mara ya kwanza nimeshuhudia ktk Gazeti la The East African linalochapwa Nairobi-Kenya ktk Ukurasa wa 12 wakiandika kuhusu Hotuba ya Kikwete wakisema...(i)''President Kikwete one of leading Economists in the region''...(ii)Kikwete says you cannot integrate while isolating''...(iii)Kikwete says Political federation cannot stand without sounding Economic foundation, if not this is waste of time''...HAWA JAMAA MARA ZOTE HAWAJA WAHI KUTOA KAULI KAMA HIYO HAPO KABLA KUHUSU KIKWETE WAO HUWA NI WAPONDAJI TU.

    2.UGANDA,
    Maoni ya wananchi wengi juu ya suala la UHAMIAJI NA AJIRA ambalo Raisi Kikwete ameligusia ktk Hotuba, huko Uganda Raisi Museveni wiki 2 zilizopita alifuta Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kenya na Rwanda wawapo Uganda, hivyo kusikia Msimamo wa Raisi Kikwete juu ya suala hilo wananchi wengi wamemlaumu Raisi Museveni na kumsifu Mhe. Raisi Kikwete.

    3.RWANDA,
    Kagame ameitisha Baraza la Mawaziri siku ya pili baada ya Hotuba tarehe 8 Novemba 2013 na kusisitiza MUUNGANO ,UMOJA NA MARIDHIANO hivyo hoja ya Utengano kama laivyosema Kiwkete ''you can't integaret while isolate'' limewaingia sana.

    Pia siku hiyo hiyo, Rwanda imetazama kurudishia Uanachama wake ktk ECCA (Umoja wa Kiuchumi wa Afrika ya Kati) walio uacha mwaka 2007, walipoulizwa Maofisa wa Serikali na Waziri wamambo ya nje wa Rwanda akasema TUNAHITAJI KUWA NA UANCHAMA NA MASHIRIKISHO ZAIDI YA MOJA PIA ''TUMEONA KTK HII AFRIKA YA MASHARIKI HATUNA SAUTI'',,,HII NI MOJA KWA MOJA WAMEONA LAWAMA ZIMEWASHUKIA KWA KUTAKA KUSHINIKIZA MAMBO KTK EAC KAM RAISI KIKWETE ALIVYOSEMA KTK HOTUBA YAKE DODOMA.

    ReplyDelete
  7. Angalieni wasije wakatufanyia ule mchezo wa daganya toto. Maneno matamu vitendo hamuna!

    ReplyDelete

  8. GOD BLESS YOU OUR DEAR PRESIDENT.
    Hotuba uliyoitoa bungeni ilikuwa imeenda shule hasa.Ilikuwa nzuri kwa kila ulichokiongea.Asante sana.
    Hawa jamaa kweli wasituendeshe hatuhitaji kuwabembeleza.
    Wanyaranda wamezoea utengano na Museveni halali kwa kuuota uraisi wa Shirikisho.
    Wengi wao wanatamani ardhi yetu,uraia na mengine mengi tu.
    Tunapenda umoja lakini wasituchagulie tunachokitaka.

    ReplyDelete
  9. Tanzania tunahitaji muda wa kutosha ili kujiridhisha ikiwa kweli Kenya wanaunga mkono msimamo wa Tanzania kupitia hotuba ya hivi karibuni ya Hon. JK kuhusu EAC.

    Kitendo cha Serikali ya Kenya kumtuma Waziri wake wa mambo ya nje Amina Mohamed haitoshi kuhitimisha kuwa eti kwa kufanyahivyo ndiyo wanaunga mkono msimamo wa TZ, no please hii inahitaji muda ili kuona kama baada ya hii hotuba (na kama kweli wameelewa) basi tutarajie waachane na hivi vikao vyao vya the so called "coalition of willing"

    Lakini kama Kenya wataendelea kuhudhuria hivyo vikao vyao sasa huu si utakuwa ni unafiki tu wa kawaida; yaani kututuliza kwa muda ili angalau jazba ishuke then tuweze kuwapigia vuvuzela huko ICC kuhusu kesi ya Rais Kenyatta....we need to monitor them very closely to see if they really mean it!

    Binafsi sipingi sana ujio wa Waziri Amina, maana at least Kenya wameonyesha kujali nafasi ya Tanzania kama mdau wa muhimu EAC na kwamba pengine wanathamini wapi EAC imetoka na nini umekuwa mchango wa TZ.....so let's give them time.

    Na kwa wakati huu wa sasa acha tuwatazame Kenya kwenye kapu lilelile la "caolition of willing" wala tusiseme kuwa hao wana nafuu hakuna....after all sijui kama Waziri Amina aliihakikishia Serikali ta Tanzania kwamba Kenya hawataendelea na hivi vikao vyao....sasa why trust them?

    Si unaona tu apoapo akakumbushia tusiache kupiga ukelele huko ICC ili kesi ya "UK" iahirishwe kwa 1 yr aweze kutumikia serikali ya Kenya.....Tuangalie kwa umakini "never trust anybody" watu wanafiki sana hawa yaani vikao vitatu Kampala, Mombasa, Kigari bado Kenya hawakujua wapo off line mpaka JK atoe hotuba?

    ReplyDelete
  10. Mdau wa 9 hapo juu,

    Hawa jamaa Kenya na Rwanda na Uganda wanaponzwa na radharau dhidi yetu Tanzania na Viongozi wetu.

    Kama anavyo sema Mdau wa 6 juu Kenya ktk Gazeti lao la The East African HAWAKUWA NA UTAMADUNI WA KUMUONGELEA RAISI KIKWETE VEMA MARA ZOTE WAMEKUWA NI WAPONDAJI, HII NI DHARAU ISIPOKUWA BAADA YA KUWASHUKIA NA KUWACHANA KWA POINT ZA UKWELI NA ZA USOMI ULIO BOBEA IKABIDI WAMKUBALI !!!

    ReplyDelete
  11. Somo wamelipata !

    Kazi ipo kwenye Kikao kijacho cha EAC itakuwa hapatoshi!

    Kikao kitakuwa cha moto sana.

    Nafikiri Mhe.Dr.Jakaya Kikwete atawachana sana zaidi huko.

    Kwa mtaji huo pana uwezekano wamekaa wote K3 na 'Coalition of willing' yao wakashauriana na ndio waka mchagua Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya aje kwa niaba yao lakini kimtindo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...