Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na
ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe
katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha
CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi sambamba na kuwahimiza
kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika
Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya
zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wananchi hao walikwenda
mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
Mbunge wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Ndugu Kinana na Ujumbe wakielekea kagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo Mh.Vita Kawawa, Katibu wa NEC, Siasa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa Wodi ya Wazazi na Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Jengo la Utawala wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo.
Barabara ya kuelekea kwenye hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM na Ujumbe wake wakipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha Wilaya ya Namtumbo.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...