Viongozi na wasomi mashuhuri wa vyama na taasisi nyeti barani Afrika wanakutana kwenye kongamano la siku mbili kujadili na kupendekeza sera zinazotekelezeka na kuzingatia mazingira ya Afrika ili kuchochea mabadiliko na kuleta maendeleo.

Kongamano hili limeandaliwa na taasisi za Club de Madrid kwa kushirikiana na UONGOZI Institue. Kongamano litaendeshwa kwa uenyekiti wa marais wastaafu na wanachama wa Club de Madrid, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Festus Mogae rais mstaafu wa Botswana.

Dhumuni kubwa la kongamano hili ni kutoa fursa kwa viongozi wa Afrika kuchambua mapungufu na vikwazo vya maendeleo Afrika na kupendekeza mifumo mbadala itakayoweza fungua kurasa mpya wa mchakato wa maendeleo.

Kongamano hili litazinduliwa na mkutano mfupi asubuhi ya tarehe 19, Novemba katika hoteli ya Serena ambapo viongozi kadhaa wa kiserikali, sekta binafsi na vyama vya kijamii wapatao 80 wamealikwa. Mkutano utaongozwa na majadiliano yenye mad ‘Leading Change for Transformation: Experiences from African Leaders’ . Marais wastaafu Benjamin Mkapa na Festus Mogae watatoa uzoefu wao katika kuongoza nchi na mapambano ya kukuza na kuboresha uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...