MAREHEMU  MZEE  SABINUS P. KWEKA 
30/12/1935 - 22/11/2004 
                                     Baba, leo umetimiza miaka tisa tokea ulipoitwa gafla Nyumbani kwetu mbinguni kwa shinikizo la damu kweli “Ua zuri limerudi kwenye Bustani ya EDEN”
Tunakukumbuka kwa mengi sana,hasa Elimu na Ucha – Mungu wako, Nakumbuka maneno yako “ Huyu adui Ujinga lazima mpigane naye na ukawa ukimwomba Mungu asichukue  roho yako hadi mtoto wa mwisho amalize shule sikumbuki pia siku tuliyolala na kuamka bila ya Kusali na kwenda Ibadani ulikuwa kiongozi mzuri wa watu kwa enzi zile za UDIWANI wako wa kata ya Machame Mashariki na Mwenyekiti  wa Baraza la Walei NARUMU kweli ulikuwa mfano wa kuigwa, kwani ulivipiga vita vilivyo vizuri,mwendo ukaumaliza na Imani umeilinda
Unakumbukwa sana na mimi mwanao wa kwanza JANE, watoto wako wengine FESTO,EUGENIA,ELIZABETH,CECILIA NA THADEI.Mkeo mpendwa URSULA,dada yako wa pekee aliyebaki SR. DEVOTHA KWEKA CDNK,WAKWE ZAKO, WAJUKUU wote pamoja na Vitukuu,Wanaukoo wa KWEKAWANARUMU, Ndugu, Jamaa na Marafiki .

MISA YA KUMUOMBEA IMEFANYIKA LEO KWENYE KANISA LA BURKA – ARUSHA NA MKOLANI MWANZA

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE

APUMZIKE KWA AMANI – “AMINA”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...