Wahitimu wa Jeshi wa Zimamoto na Uokoaji wa kozi ya kuzima moto wa ndege wakizima moto kwenye ndege bandia kabla ya mafunzo yao kufungwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Maofisa na Askari 21 wa jeshi hilo walihitimu mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahitimu na wageni waalikwa kabla ya kufunga mafunzo ya kozi ya uzimaji moto wa ndege. Maofisa na Askari 21 walihitimu kozi hiyo na kutunukiwa vyeti katika sherehe fupi ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha. Kulia ni Meja Generali Kapwani, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga.
 

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi zawadi ya cheti mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo darasani, Mohammed Shomari (kulia). Akizungumza baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliomaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege, Waziri Nchimbi aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu kazi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
 
 Kikosi cha gwaride la wahitimu kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege kwa maofisa na askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliohitimu kozi hiyo jijini Dar es Salaam leo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye aliyafunga mafunzo ya kozi hiyo aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu kazi.
 
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha, akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) kwa kukubali wito wao wa kuja kuyafunga mafunzo ya Maofisa na Askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliohitimu mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege. Waziri Nchimbi katika hotuba yake aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu kazi. 
Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. maafisa hao wanaozima moto hawajavaa cha helmet (hard hat) wala gloves. moto gani huo watazima.

    hata kama ni demo, bado kuna umuhimu wa kuvaa hizo protection kujenga mazoea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...