Marehemu Mama Leonia Ireneus Shirima

Mama yetu Mpendwa, leo umetimiza miaka saba (25 Novemba 2006) tangu ulipoitwa ghafla na Mwenyezi Mungu aliye juu Mbinguni na mkuu na muweza wa yeto duniani na mbinguni. Hakika ua zuri limerudi kwenye bustani ya Eden.

Tunakukumbuka kwa mengi sana hasa malezi bora kwetu, elimu, ushauri, ucha Mungu na mengine mengi.
Kila mmoja wetu, kwa namna ya kipekee, anakumbuka upendo wako wa dhati kwetu sisi wote, wanao na wakwe zako bila ya ubaguzi wowote. Upendo wako kwetu umekuwa nuru na mfano wa kuigwa nasi na umetufanya tushikamane na kupendana sana na tunamuomba Mwenyezi Mungu ili tudumu kwenye mshikamano na upendo huo.

Unakumbukwa sana na mumeo mpendwa, Mzee Ireneus Shirima, watoto wako – Joseph, Archady, Jerome, Clotilda, Eusebia, Florid, Flavia na Clemence pamoja na wakwe zako - Irene, Rose, Mariam, Francis, Salvatory, Lilian, George na Neema. Unakumbwa pia na Easther pamoja na wajukuu zako wote, ndugu,jamaa na marafiki.

RAHA YA MILELE UMEPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWAANGAZIE.
APUMZIKE KWA AMANI, AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...