Na Ally Kondo, Kuwait

Serikali ya kuwait imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni moja (1) kwa ajili ya kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Tangazo hilo lililotolewa na Amir wa Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu (Third Afro Arab Summit), Sheikh Sabah Al-Ahnad Al-Sabah wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi ya mkutano huo nchini Kuwait siku ya Jumanne tarehe 19 Novemba, 2013.

Sanjari na kiasi hicho cha fedha, Sheikh Al-Sabah alitangaza kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni moja (1) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za utafiti zenye lengo la kuibua fursa za maendeleo katika nchi za Afrika.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. tanzania pekee inaweza kuwa na zaidi ya dola bilionni kumi (USD 10 Billion) kila mwaka. Vyanzo ni umiliki vyema wa mali zetu na kukusanya kodi vyema kwa kila anayepata fedha kupitia tanzania. Sasa angalia kainchi kadogo kanatoa dola bilioni moja kwa nchi zaidi ya 50 za afrika. Afrika yenye mali ambayo yaweza lisha dunia nzima inakuwa ombaomba; tuchape kazi ndugu zangu; la zivyo tutakuwa manyapala na watumwa wa wakoloni. kumbuka nchi za ulaya walikaa mwaka 1884 kuigawa afrika ndani ya himaya yao; hatujui wamepanga nii juu yetu. Watu wa usalama wa nchi yetu na bara letu la afrika wanaweza kutuelimisha.

    ReplyDelete
  2. Afrika sasa hivi ina marafiki wengi wanaotaka kutoa mikopo kila mahali, bara hili lisipokuwa makini na kuchukua mikopo kwa vitu vya lazima tu kama ujenzi wa miundo mbinu basi itakuwa ni kulipa mikopo kwa muda mrefu. Tuwe makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...