Mfuko wa pensheni wa LAPF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania
wenye makao makuu yake Mjini Dodoma, umekabidhi vifaa vya michezo
vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa Chama cha
michezo cha Vyuo Vikuu vya Tanzania TUSA, kwa ajili ya mashindano ya
TUSA yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 10 - 17 Desemba,
2013.
Sherehe fupi ya makabidhiano, imefanyika katika Ofisi za LAPF,
zilizoko Millennium Towers jijini Dar es Salaam.
Meneja wa
LAPF Kanda ya Dar es Salaa, Bibi Amina Kassim, amesema Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umekuwa pia ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii
katika kusaidia sekta mbali mbali kama elimu, hospitali, vituo vya
kulea watoto yatima na pia katika sekta ya michezo kusaidia kuinua
michezo nchini.
Bibi Kassim amesema, hii ni mara ya tatu kwa LAPF kudhamini mashindano
kwa mara ya kwanza LAPF ilidhamini mashindano ya mwaka 2011 na 2012,
ambapo LAPF imetoa vifaa hivi kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi wa
taasisis hizo kama wanachama wetu watarajiwa.
Amesema kufuatia LAPF kuwa Mfuko bora wa Pensheni kwa kudhihirishwa
kwa tuzo iliyotolewa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii SSRA
kuwa LAPF kuwa ni Mfuko wa Pensheni unakua kwa kasi Zaidi nchini.
Kitendo cha LAPF kuwa imekuwa ikipata tuzo kutoka kwa bodi ya
wahasibu nchini NBAA kwa kuwa Mfuko wenye Hesabu Bora za mwaka kwa
miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008, 2009, 2010 na 2011, LAPF
sasa imeamua kujikita kudhamini michezi, ili kurudisha kwa jamii,
sehemu ya mafanikio hayo.
Akishukuru kupata vifaa hivyo, Mwenyekiti wa TUSA Taifa, Asnati Chagu
aliishukuru LAPF kwa msaada huo, na kusema umekuja wakati muafaka, ila
pia akaomba wafadhili wengine wazidi kujitokeza ili kufanikisha
michuona hiyo.
Amesema msaada huoiwa jezi ni moja tu ya mahitaji, lakini bado kuna
mahitaji mengine yanahitajika vikiwemo vikombe na zawadi kwa washindi
mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...