Assalam ´alaykum warahmatullaahi wa Barakatuh

       Karibuni nyote katika tovuti yenu:


Tunayo furaha kubwa ya kuwajulisha ndugu zetu Waislamu ya kwamba, kwa hivi sasa tumeafikishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kufungua Tovuti maalumu ambayo ni khaswa kwa Wanachuoni tu baada ya maombi ya muda mrefu kutoka kwa baadhi ya ndugu kutokana na uzito waliokuwa wakipata pindi wanapotafuta aitha Fatwa, kitabu au makala; kwani vitu hapo kabla havikuwa sehemu moja na haikuwa sahali kupata kile anachotafuta mtu.

Tovuti yetu tumeonelea kuipa jina la: Wanachuoni.com kutokana na sababu zifuatazo:
1) Hakuna kitachowekwa isipokuwa tu kazi mbalimbali za Wanachuoni - sawa waliotangulia na walioko hivi sasa.
2) Sisi kazi yetu ni kutarjumu (kufasiri) tu zile kazi za Wanachuoni; kama vitabu, makala na fataawa. 
3) Usahali wa jina hili, sawa katika kuliandika na kulikumbuka.

Hizi ndizo sababu tatu kuu kuchagua jina hili.

Katika moja ya matunda, natija na faida tunayopata kutoka www.alhidaaya.com mpaka hivi leo, naweza kusema ya kwamba ni pamoja na hivi leo kupatikana Tovuti yenu hii www.wanachuoni.com. Nimesema hayo kutokana na sababu nyingi tu. Hatuna cha kuwalipa wahusika wote wa Alhidaaya zaidi ya kuwaombea Du´aa na kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Azidi kuunufaisha Ummah kupitia tovuti hizi.

Tunachowaomba ndugu zetu ni kuzidi kuwa na subra, kwani tumewaandalia vitu vingi vya Wanachuoni ambao ndio warithi wa Mitume (´alayhimus-Salaam), kukiwemo: vitabu, makala na fatwa ambavyo vimeshakuwa tayari na imebaki kuviweka tu kwenye Tovuti.

Tunaomba msitusahau katika Du´aa zenu za kila siku. Na kila yule mwenye maoni na ushauri juu ya Tovuti yenu hii, tunaomba asikose kutuandikia kupitia kwenye tovuti Wanachuoni kwa juu - kipengele kinachoitwa ”Wasialiana nasi” au kupitia email yetu hii.

Allaah Awajaze kheri nyote.

Ndugu zenu wa:
Wanachuoni.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aliyetuummba awaongoze na awape malipo yaliyoyakheri kutokana na yale muyafanyayo kwa ajili Yake tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...