Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi. 
 TAARIFA zinaonesha kuwa Mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji hapa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya Wanawake 100 wanaotoka katika mkoa huo 71 wamefanyiwa ukeketaji. 
 Akitoa taarifa za utafiti huo katika siku ya uzinduzi wa Maadhimisho ya kimataifa ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zinazofanyika kikanda mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Mtandao wa kuelimisha Jamii juu ya madhara ya Ukeketaji (NAFGEM), Francis Selesini alisema kuwa tafiti hiyo inaonesha kuongezeka kwa vitendo vya ukeketaji. 
 Selasini alisema katika Utafiti huo uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na shirika la kimataifa linaloshughulika na na watoto (UNICEF) kuhusu athari ya vitendo vya ukeketaji, taarifa zinaonesha kuwa Mkoa wa Manyara unaongoza kwa matukio ya ukeketaji ambapo kati ya wanawake mia moja, 71 wamekeketwa. “Tafiti mbambali zilizofanywa zinaonesha matukio ya ukeketaji kuongezeka hasa katika Mkoa wa Manyara ambako kati ya wanawake mia, 71 kati yao wamekeketwa, hili ni tatizo kubwa sana,” alisema Selasini. 
 Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika msururu huo pia imebainika kuwa mkoa wa Dodoma ambayo ni makao makuu ya Tanzania Inafuata ambapo kati ya wanawake mia moja, taarifa zinaonesha 60 kati yao wamefanyiwa kitendo hicho cha kikatili. 
 Aidha kuhusu Taarifa za kikanda Selesini aliitaja Kanda ya Kati inayoundwa na mikoa ya Singida na Dodoma, kuwa kinara wa vitendo vya ukeketaji wa wasichana ambapo kati ya wasichana mia moja, taarifa zinaonesha kuwa 50 kati yao kufanyiwa vitendo hivyo. 
 Kanda ya Kaskazini, inayoundwa na mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, ni ya pili kwa matukio ya hayo ambapo kati ya wanawake mia moja, 35 wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji. 
 Hata hivyo moja ya sababu za kukithiri kwa matuki hayo Mkoani Manyara, mkoa unaoundwa kwa asilimia kubwa na Jamii ya Wafugaji, ilidaiwa kuwa ni mila na Desturi ya watu wa maeneo hayo ambao wengi wao ni jamii ya Kimaasai ambapo Ukeketaji kwa imani zao inaonekana kama sehemu ya mila na Desturi na bila ya kufanya hivyo mwanamke huchukuliwa kama Mtu ambaye bado hajakomaa.
 Changamoto nyingine zinazokabili mapambano ya kupinga ukatili huu ni swala la Mfume Dume ambayo kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha kuongezeka kwa Ukeketaji kwani wanawake wa maeneo hayo huwa hawana sauti ya kuzungumza na kukemea kile ambacho wao wanakiona kama kikwazo kwao.

 Maandamano kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yalivyofanyika mjini Moshi
 Afisa uhusiano wa shirika la KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ,Jaji Aisha Nyerere wakati wa maonesho yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa YMCA.
 Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazoshiriki katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Jaji Aisha Nyerere.
 
 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Jaji Aisha Nyerere akitoa hotuba katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.

Maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yalivyofanyika mjini Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wao! maandamano yamefanyika kwenyewe. Mie nilikataa kuolewa kwetu sabb hiyo hiyo.....Eee Mungu, geusa mioyo ya watu wapende wake zao kama wenzao sio matrakta.

    ReplyDelete
  2. Magomvi nyumbani siku hizi yamesababisha hata wanawake kupoteza maisha. Mwanamke anapoona maisha yake yamo hatarini kwa sababu ya kutishiwa,kupigwa na kukosa amani atoke asingoje kumalizwa. Hii inatakiwa wanawake pia wajiendeleze ili wapate pa kwenda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...