Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya akizungumza na wadau wa sekta mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye ambaye alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mchango wa takwimu katika kufanikisha majukumu ya Jeshi la Polisi nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Amesema kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu mengine inaendelea kuhimiza matumizi ya takwimu kutoka katika vyanzo sahihi kwa mipango ya maendeleo.

Muimbaji maarufu nchini Tanzania Bi. Stara Thomas akiwasilisha ujumbe kwa njia ya uimbaji kuhusu umuhimu wa matumizi ya Takwimu katika kupanga mipango ya Maendeleo leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni zinazohusu nyumba bora kwa mfano na umeme zinaonyesha inabidi tuongeze kazi katika ujenzi wa nyumba bora kama njia ya kujiletea maendeleo.
ReplyDelete