Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam
kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa majadiliano ya wawekezaji wa kitaifa na
kimataifa mwezi huu.
====== ======= ========

Maandalizi
ya mkutano ya majadiliano ya wawekezaji ya kitaifa na kimataifa kwa
upande mmoja na serikali kwa upande mwingine inayotarajiwa kufanyika
mwezi huu inaendelea vizuri.Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi
aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa
Kinachofanyika sasa ni maandalizi ya mada ya nini kitazungumzwa wakati
wa mkutano.TNBC ndio wanaoratibu mkutano huo.
“Mada
ya kwanza ni mazingira ya biashara…kuna kikundi kazi kinachotayarisha
mada hii kwa kuangalia maeneo yanayotakiwa kuboreshwa na serikali ili
sekta binafsi iweze kufanya biashara vizuri,” alisema Mbilinyi. Alisema
kikundi kazi hicho kinachoundwa na wadau toka sekta binafsi na umma
sasa kinapitia maeneo mbalimbali ambayo ni muhimu kujadiliwa na pia
kuangalia ripoti mbalimbali za kimataifa zinavyoonyesha jinsi Tanzania
inavyopimwa.
“Kuna maeneo tunayofanya vibaya lakini pia kuna maeneo tunayofanya vizuri. Sekta
binafsi itakuja na mapendekezo yake na kujadiliana na sekta ya umma na
kisha kuangalia jinsi ya kuboresha maeneo hayo,” alisema Mbilinyi. Alisema
eneo la pili linalotarajiwa kuongelewa ni mpango wa ‘Matokeo Makubwa
Sasa’ ambalo serikali imejipima na kujipanga vizuri kufikia uchumi wa
kati mwaka 2025.
“Moja
ya mambo yatakayojadiliwa ni ushiriki wa sekta binafsi katika
kutekeleza vipaumbele katika mpango huu wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’. Mkakati
huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi Februari mwaka huu
unalenga kufikia malengo katika vipaumbele vya maendeleo ya nchi kwa
muda maalum ambapo viongozi wanatakiwa kuonyesha walichofanikisha.
Vipaumbele vya mkakati huo wa serikali ni pamoja na elimu, nishati, kilimo, usafiri, maji na maendeleo ya raslimali watu.Kwa mujibu wa Bw. Mbilinyi eneo lingine litakalozungumziwa ni eneo la uwezeshaji kwa mapana yake. “Sekta binafsi ni kubwa nchi hii. Tutaangalia
utaratibu gani serikali iweze kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha
kuwa swala zima la maendeleo na uchumi linahusisha uwezeshaji,”
alisema.
Mikutano
hiyo ilianza kufanyika mwaka 2003 ikishirikisha wawekezaji wa ndani na
wa nje kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine kwa malengo ya
kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji kwa manufaa ya
pande zote mbili.
Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) ndilo lenye dhamana ya uandaaji wa mikutano hiyo kwa miaka 10 sasa.Mikutano hii ilianzishwa kuwa kama jukwaa la kubadilishana uzoefu katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...