vizuri Worldwide. Muziki wake unazidi kusambaa katika wigo wa Dunia
sasa, sio Afrika tu. Uwezo wake wa kuchana kwa lugha ya Kingereza na
Kiswahili unamnyooshea wigo huo pia.
Ni juzi kati tuu mrembo huyo aliyebarikiwa kipaji cha kurap vizuri
aliachia wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Producer Dunga. Wimbo
huo umepewa jina la Lets Wait na ulitengenezwa kwenye studio za
Fishcrab cookout.
Lets Wait ni wimbo mzuri sana kiasi cha kufanya baadhi ya mashabiki wa
Cindy Rulz kuhisi kuwa huo ni wimbo mkali kuliko zote alizowahi
kufanya. Pongezi liende kwa Producers, Lamar na Dunga ambao kwa kiasi
kikubwa pia wamefanya wimbo huo kufika levels ilipo sasa.
Kwanza kabisa Lyrics za wimbo huo zimekuwa certified na Rapgenius, kwa
maana hiyo mashairi ya wimbo huo yanapatikana kwenye website kubwa ya mashairi nchini Marekani, Rapgenius.com ambayo inatembelewa na mamilioni ya watu kila siku.
Mtu wa kwanza hapa Bongo kusikia akiwa amewekewa mashairi kwenye
mtandao huo ni Gosby, sasa Cindy Rulz nae amemanage kufika huko na
naamini hizo ni juhudi binafsi ili kuweza kufikisha wimbo katika level
za kimataifa. Naamini watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanasoma
mashairi ya Lets Wait na kusikiliza audio so that they can sing along
at the same time kwasababu mtandao huo unaruhusu kufanya hivyo.
Sasa katika katika pitapita zangu nikakutana na blog moja, Death
Chambers Music ya Marekani ikiwa inauzungumzia wimbo huo huo wa Lets
Wait. Mwandishi wa habari hiyo alikiri kwamba haelewi moja kwa moja
kilichozungumziwa kutokana na mchanganyiko wa lugha, Kingereza na
Kiswahili ila aling'amua kwamba kinachozungumziwa ni mapenzi. Lakini
mwandishi huyo pia hakuweza kujizuia kumsifu Cindy Rulz kwa jinsi
alivyoweza kupita vizuri kwenye beat ya wimbo huo.
Anyways, Cindy hakuishia hapo kwani siku chache baada ya kurelease
wimbo huo mpya akaachia video ya wimbo wake uliopita, Utanifanya
Nighairi ambao amemshirikisha Chidy Bway. Ngoma ilifanywa pale G. Recs
kwa KGT, honestly naukubali sana huu wimbo.
Kitu kizuri kuhusu hii video ni jinsi ilivyopokelewa vizuri na
mashabiki wa muziki wa Bongo Flava. Lakini kizuri zaidi ni pale
mtandao mkubwa wa Marekani tena viewhiphop.com kuupromote au kuupa
shavu kwa kuitupia video hiyo kwenye mtandao wao, bonge la zali sio?
Naamini ukiwa na juhudi binafsi kama msanii lazima utafika mbali tu.
Cindy Rulz ni msichana anayejua kurap na anafanya muziki mzuri,
mwenyewe anakwambia classic music, yuko serious na anachokifanya na
yupo kwenye management nzuri pia. So naamini juhudi zake zitamfikisha
mahala anapopataka, atakuwa msanii wa kimataifa kama anavyojijenga
sasa.
Haya ni mafanikio ambayo wasanii wengi wa Bongo hawayapati na matokeo yake wanaishia kusikika hapa hapa nyumbani. Mafanikio haya pia yanarahisisha collabo na wasanii wakubwa duniani kwa sababu muziki
wako utasikilizwa na watu wengi wa nchi tofauti tofauti na kufanya
muziki wako kukua zaidi.
Kwa hapa nyumbani, Cindy Rulz amepata Interviews zakutosha karibu
kwenye Radio zote za Dar es Salaam na TV stations tangu ameachia audio
na video za Lets Wait na Utanifanya Nighairi respectively.
Hongera Cindy, now you are rocking on Keezywear.com na endelea
kuwakilisha muziki wa Tanzania duniani kote! Endelea kurequest nyimbo
za Cindy Rulz on your favorite Radio na TV!
Like Keezywear on Facebook!
Follow @keezywear on Twitter!



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...