CHUO Kikuu Cha Kiislamu Cha Morogoro kimefanya Mahafali ya sita leo katika viwanja vya michezo ndani ya eneo la chuo. Jumla ya wahitimu 814 walihudhuria mahafali hayo ya sita na kutunukiwa shahada ya kwanza katika kozi mbalimbali.
Katika shahada ya sanaa na ualimu walikuwa wahitimu 599 waliotunukiwa shahada siku ya leo, shahada ya sanaa na mawasiliano ya umma wahitimu 20, shahada ya lugha na ukalimani wahitimu 6, na shahada ya maarifa ya kiislam na ualimu wahitimu 61
Wengine ni kwenye shahada ya biashara wahitimu 13, shahada ya sayansi na ualimu 99 na shahada ya sheria na sharia’h wahitimu 16. Mgeni Rasmi kwenye mahafali haya ya sita alikua ni Mkuu wa chuo Hajjat Mwatumu J.Malale, vilevile alikuwepo Dr M. J Assad Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu na Prof Hamza Njozi Makamu Mkuu wa Chuo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa na furaha na fahari baada ya kula nondozzzzzz zao leo
Kinadada wakipozi baada ya kula nondozzzzz
Picha ya pamoja baada ya kula nondozzzzz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kila la kheri, mukatumikie taifa. Wananchi wanawasubiri

    ReplyDelete
  2. mjitahidi hivyo hivyo ndugu zangu msirudi nyuma elimu ndo msingi wa maendeleo na msisahau dini yenu na wapi mlipotoka na mnataka kwenda wapi Allah peke ndo mkimshika hatokupotosheni ni kamba imara mshikeni sana na dini yenu msiifanyiye mchezo hata kidogo hata siku mmoja wenzenu wanalijua hili na nyinyi lazima mlifahamu hili msiyumbishwe na dunia na kuitupa dini yenu kisa tu mmepata elimu never never again.

    nakutakiyeni kila la kheir na barka tele na Allah akulindeni na akukuzeni na akujaliyeni kila la kheir amin amin amin.

    nimefurahi sana kuona kina dada zetu wanavaa hijaab na kwa kweli wamependeza sana mashallah

    hongereni sana kwa mafanikio yenu ya kusoma na kuhitimu Allah daima awe na nyinyi amin amin amin.

    mdau majuu anayekutakieni kila la kheir na ahsante michuzi kuweka picha hizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...