Wakala wa M-pesa wa Wilayani ya Bunda Godfrey Morice akionyesha cheti na mfano wa ujumbe alipupokea kwenye simu yake kumjuliusha kupokea Sh 100,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi watano wa droo ya promosheni ya Mkwanja kwa Wakala kwa wilaya ya Tarime. Promosheni hiyo inaendeshwa kwa mawakala wa M-pesa nchi nzima. Kushoto ni Meneja wa Vodacom Tarime na Bunda Stide Tibenda.
Mfanyakazi wa Duka la Vodacom Dodoma David Ganya akimkabidhi wakala wa M-pesa Dodoma Veronica Asei mfano wa ujumbe wa simu alioupokea baada ya kushinda Sh. 100,000 kwenye droo ya wiki ya promosheni ya Mkwanja kwa Wakala. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa duka hilo wakiongozwa na Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati Mruta Hamis (wa pili kulia). Promosheni hiyo inawahusisha mawakala wa M-pesa nchi nzima.
Wakala wa M-pesa Ibrahim Shetwani wa mjini Dodoma akipokea mfano wa ujumbe wa simu alioupokea kwenye simu yake ya mkononi baada ya kushinda S. 100,000 kwenye droo ya wiki ya promosheni ya Mkwanja kwa Wakala. Promosheni hiyo inaendeshwa kwa mawakala wa M-pesa nchi nzima.
Meneja wa Vodacom Geita George Venanty akimkabidhi mshindi wa droo ya Promosheni ya Mkwanja Kwa Wakala Mery Ponda mfano wa ujumbe wa simu alioupokea kwenye simu yake ya mkononi baada ya kushinda Sh. 100,000 kwenye droo ya wiki ya promosheni hiyo. Mshindi huingiziwa moja kwa moja kwenye simu yake fedha ya ushindi kwa njia ya M-pesa Anaeshuhudia ni Veronica Godfrey. Promosheni hiyo huwahusisha mawakala wote wa Mpesa nchi nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...