Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikamilisha ahadi yake ya kuchangia Elimu kwa Shule za Sekondari Mbagala,kwa kumkabidhi Mchango wake wa Sh. Mil. 10,Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario (wa tatu kulia).Wengine pichani ni Walimu wa Shule mbali mbali za Sekondari zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala.Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario (aliesimama) akisoma taarifa fupi ya namna walivyoweza kuiendesha harambee ya kuchangia Maendeleo ya Elimu katika Tarafa ya Mbagala,iliyofanyika majuma kadhaa yaliyopita.wakati walipofika Ofisini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,kuwasilisha taarifa hiyo leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea taarifa hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na walimu hao mara baada ya kuwakabidhi mchango wake leo,Ofisini kwake.
Baadhi ya wakuu wa Shule mbali mbali za Sekondari katika Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Mh. Lowassa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...