Na Rashid Mkwinda
Ligi Kuu ya Bara imeendelea leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na wenyeji Mbeya City imeshinda kwa goli 1-0 lililopatikana kwa mchezaji wa timu ya Ashanti Samir Rubava kujifunga katika dakika 30 ya mchezo.
Ashanti walioonesha kuutawala vyema mpira tofauti na wenyeji Mbeya City, walifanya mashambulizi mengi katika lango la Mbeya City lakini safu ya mashambulizi iliyoongozwa na wachezaji Farihi Rashid,Husein Sued na Joseph Mahundi ilionekana kushindwa kuelewana katika umaliziaji.
Dakika ya 18 ya mchezo nusura Ashanti ijipatie bao baada ya golikipa wa timu ya Mbeya City David Burhani kutoka golini huku shuti lililopigwa na mshambuliaji wa Ashanti Joseph Mahundi likiambaa ambaa golini kwa Mbeya City ambapo mchezaji wa timu ya Mbeya City Antony Matogolo alikimbilia mpira huo na kuoondosha ukiwa unakaribia kuvuka mstari wa goli.
Hadi mapumziko na hata baada ya dakika 90 Mbeya City ilitoka kifua mbele kwa goli 1-0.
Mbeya City iliwakilishwa na wachezaji David Burhani, John Kampambe,Hamad Kipobile/Richard Peter,Degratious Julius,Yusuf Abdallah,Antony Matogolo,Alex Seth,Steven Mazanda,Paul Nonga/Yohana Morris,Francis Casto/Mwagane Yeya na Hassan Mwasapili.
Ashanti United iliwakilishwa na Amani Simba,Antony Vicent,Khan Alex,Tumba Lui,Samir Rubava,Idd Sailas/Abdul Kumbilwa,Farihi Rashid,Mussa Mohamed,Paul Maona,Husein Sued/RichardLyangile na Joseph Mahundi.
Ashanti United kabla ya mchezo wao na Mbeya City
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...