Waandishi wa Habari kutoka Tanzania na Kenya wakimsikiliza Muongozaji wa Watalii katika Makumbusho ya Hector Pieterson (Mtoto aliyekufa kwa kupigwa risasi wakati wa kutafuta haki ya Mwafrika nchini Afrika Kusini) aitwae Antoinette Sithole (kulia) ambaye pia ni Dada wa Hector Pieterson na wanaonekana kwenye picha ya chini hapo wakikimbia.Aliembeba Hector alitambulika kwa jina la Mbuyisa Makhubo ambaye hajulikani alipo mpaka leo hii toka siku hiyo.Hector Pieterson na Antoinette Sithole wote walikuwa ni Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Phefeni,iliopo Orlando West, Soweto,Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.Waandishi hao wapo nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo nchini humo kwa Mwaliko wa Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini.
Hii ndio picha pekee yenye Kumbukumbu ya Hector Pieterson akiwa amebebwa na  Mbuyisa Makhubo huku wakikimbia pamoja na Dada wa Hector aitwae Antoinette Sithole. Picha hii ilipigwa na Mpiga Picha maarufu wa Johannesburg newspaper The World, Sam Nzima.
Dada wa Hector Pieterson ambaye kwa sasa anafanya kazi ya katika Makumbusho hayo,Antoinette Sithole (wa pili kulia) akitoa maelezo ya kumbukumbu yake siku mdogo wake alipopigwa risasi mnamo mwaka 1976,wakati huo yeye alikuwa na umri wa miaka 17. Wanaomsikiliza toka Kulia ni Othman Michuzi,Pumla Dabula (kutoa Bodi ya Utalii wa Afrika Kusini) pamoja na Anganile Mwakyanjala.
Jiwe la msingi la Kumbukumbu ya Hector Pieterson.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aise Asante kwa Mapicha,nimepata kumbukumbu nzuri sana.Na mimi nilishawahi kutembelea hiyo nyumba aliyoishi Mzee Mandela,2001.Watalii walikuwa wengi sana.kumbe hadi leo bado ni "nyomi".

    Kwa ujumla Afrika ya kusini ni pazuri ila suala la ubaguzi liko pale pale.Wakati wa ziara yangu hii nilibahatika kusafri hadi mji mmoja unaitwa Barberton,nikafikia hotel moja inaitwa Phoenix.Basi jioni nikiwa kwenye mgahawa napata Kinywaji akaja mzungu mmoja akaniambia 'you Black P*%#?$..what are you doing here'?.Binafsi siku-mind sana ila wale waafrika kusini weusi waliokuwa pale walisikia yale maneno wakamjia juu yule Kaburu, kukatokea vurugu sana pale hotelini ingawa baadae palikuja kutulia..Dhambi ya Ubaguzi ni kama kula nyama ya.....WaTZ tusibaguane.Ni noma

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...