• KWA WASUKUMA WOTE DUNIANI 
    Kuna mdada anaitwa HAPPYNESS KASIL anautafuta ukoo wa mama yake mzazi kwani haufahamu.Mama na baba yake wote ni kabila la wasukuma,mama yake amezaliwa NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA.Baba yake amezaliwa NYANGUGE –BARIADI –SHINYANGA.Mama yake anaitwa MATHAR DANIEL.Baba yake anaitwa KASIL SANAGU MAJAB.Mama yake alifariki mwaka 2001.Baba yake pia alifariki mwaka 2010.Katika familia yao walizaliwa watoto sita 1.Charle Kasil 2.Happyness Kasil 3.Faustn Kasil 4.Daniel Kasil 5.Mariam Kasil 6.Neema Kasil Wamefariki watoto 3 na wamebaki 3 .Waliofariki ni Charle Kasil ,Mariam Kasil na Neema kasil.Waliobaki ni Happy kasil. Faustn kasil na Daniel Kasil.Wazazi wake walikuwa wanaishi NYARUGUSU GEITA –MWANZA.Baba yake alikuwa akinunua dhahabu Nyarugusu na anauza MWANZA.Mama yake alikuwa mama wa nyumbani.
    Mama yake alisoma shule ya sekondari NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA na kuhitimu form 4.Anamfahamu mama yake mkubwa anaitwa ESTHER DANIEL alikuwa anaishi MWANZA sasa hivi hafaamu alipo.
    Shangazi zake ni SALOME SANAG na LUSIA SANAG.Salome alikuwa anaishi MSOMA na Lusia alikuwa anaishi NGULYAT.Bibi na babu mzaa baba walikuwa wanaishi NYANGUGE BARIADI.Jina la ukoo wa baba yake ni SANAGU MAJAB.Kwa sasa Happy na wadogo zake wanaishi SIRARI9mpakani mwa Tanzania na Kenya) .
     Anaomba mtu yoyote anae ujua ukoo wa mama yake amjulishe kwa namba zifuatazo (+255 782 781834) au facebook anatumia jina la (happyness marco)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Anatafuta ukoo wa mama yake; au ndugu wa ukoo wa mama yake?? Maana ukoo tu utamsaidia nini; hasa hasa kwa sasa tunapoongelea dunia kuwa kijiji; ukoo si ni kama tone ndani ya Bahari ya Hindi jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Operation kimbunga inatufunza mengi sana hasa sisi tunaokaa / tuliozaliwa mipakani

    ReplyDelete
  3. Pole sana Happy. Kwa kuwa ana facebook account basi itakuwa vizuri kupeleka huko tangazo. Ninaamini Facebook ina mtungo wa watu wengi kwa hiyo habari inaweza kusambaa.

    ReplyDelete
  4. Nahisi unaanza kutapa tapa kabla ya KIMBUNGA hakijakufikia,na nyie wasukuma kama ndio mnavyopoteana kwanjia hiyo AIBU KWENU hii ni karne ya 21,amkeni kidogo jamani,,nahisi mnaishi katika maisha ya ASIYE SIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU huyo tayari yashamkuta ndio maana anaanza eti natafuta ukooo wangu yaani anaishi maisha ya kinyumenyume,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 2 juu,

    Sawasawa kabisa Opresheni imetufunza mengi la zaidi ni kuutambua Ukoo na Nasaba zetu.

    Mdau Happy anatetea Uraia wake wa Tanzania ya sasa ya Raisi Kikwete ya kama mjuavyo kwa sasa Uraia wa Tanzania una thamani ya juu kama wa Majuu !!!

    ReplyDelete
  6. Katika adhabu zote 9 ya 10 ni Operesheni Kimbunga ikikuelekea na ukakosa hata ndugu wa kunyooshea kidole kwamba unao Unasaba na Ukoo wowote hapa Tanzania.

    Ndio anachotafuta Mdau ndugu yetu Happy ili akiwa ameungana na Ukoo wake ataweza kujitetea kuhusu Uraia wake atakapofikiwa na Vijana wa Dr.Nchimbi huko Mpakani mwa Tanzania na Kenya hapo eneo la Sirari !

    ReplyDelete
  7. Pole,nenda huko mama yako aliko zaliwa uliza kijiji gani alitokea,maana siyo watu wote wako kwenye dunia ya digital,kama hutapata, hiyo ni wilaya watakuwa na record ya vizazi na vifo japokuwa nchi yetu bado iko nyuma kidogo kutunza record kama hizo.lakini hilo jina la ukoo wako ukiwaambia wataangalia toka enzi ya mkoloni kama aliwahi kupiga kura au aliwahi kufungwa jela etc.

    ReplyDelete
  8. Watu mna majibu mabaya sijawahi kuona kwa kuwa nyinyi ndio mnahaki sana na hii dunia au? Hamjui Mungu anaweza kuwageuzia kibao dakika moja?? Kamu huwezi kumsaidia wala kumfariji ni bora ukasoma kimyakimya. Ni Kaka yangu Michuzi comments za kuumiza kama hizi si vema kuziachia hata kama zinaukweli ndani yake. Msijihesabie haki jamani Muogopeni Mungu.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 8 hapo juu.

    Tunatoa COMMENTS ZA KUUMIZA ili watu waamke na kuuthamini Uraia wa Tanzania ya Jakaya Kikwete waliyokuwa wanaidharau kwa miaka mingi nyuma.

    Ni wakati sasa kuuthamini Uraia wa Tanzania kama mnavyoona Jirani zetu na COALITION OF WILLING yao (Rwanda, Uganda na Kenya)wamefikia kututenga Tanzania ktk Vikao baada ya kuona tumewashitukia, walipo anzia wamekuwa wanalazimisha sana huku waki harakisha tuwe na Pasipoti moja na sisi Tanzania ni kuwa kwa ujanja wao wametambua THAMANI YA URAIA WA UMOJA NA WATANZANIA!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...