Photo0001
KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA LIMITED (MeTL) Makao Makuu inatangaza kwa umma wa watanzania kwamba Meneja wa MeTL tawi la Iringa Mr Aamir Iqbal anatafutwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi wa mamilioni.
Mr Iqbal (pichani juu) aliyekuwa Meneja wa tawi la MeTL Iringa anatuhumiwa kwa kosa la kumwibia mwajiri wake mamilioni ya pesa na yeyote atakayewezesha kukamatwa au kutoa taarifa zake katika kituo chochote cha Polisi zawadi nono itatolewa.
Tukio hilo lililotokea jana mchana Iringa na limeripotiwa Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na RB ya Polisi ni ref no. IR/RB/7229/2013.
Kampuni ya MeTL Group itatoa zawadi nono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwake.
Au piga simu namba: 0755 030 014 , 2118930/1, 0713 324 332, 0715 030 024
PASSPORT AAMIR IQBAL  
Hati ya kusafiria ya Aamir Iqbal.
RPB AAMIR IQBAL  
Kibali cha kazi cha Meneja huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Huyo amesha chukua Mtaji anaweza kuondokea kupitia Afrika Kusini kwa sababu kwa Matanzania ama mwenye Kibali cha Kukaa hapa ama Kazi anaweza kwenda South bila viza.

    Pia kama mtachelewa na sasa atakuwa 'Shamba ya Kusini' muwasiliane na Ubalozi wa SOUTH AFRICA na pia Ubalozi wa Brazil hapa Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Wewe Mohamed Enterprise umezidi kuajiri watu toka nje na kudharau watanzania ! Acha wakuibie tu si ulio watu hao ni bora sana kwako kuliko kuajiri ata watu wa ndani !

    Tunasikitika sana kwa kutojali watu wa ndani katika kampuni zako katika nafasi za juu umejaza watu wa nje tu.

    Wape usawa na tanzania kuliko watu wa nje unavyowadhamin.

    ReplyDelete
  3. Sasa inashangaza jamani,huyu mpakistan alikuwa anaishi nchini kama meneja,wakati hapa tunao watoto wetu wenye elimu ya kutosha kufanya kazi hiyo?
    Pole sana kwa kuibiwa
    lakini jaribu kuwapa ajira watanzania wenzio kuliko kutoa ajira
    kwa vigezo vya rangi ya ngozi

    ReplyDelete
  4. walikosa watanzania kufanya hiyo kazi? tujiulize!

    ReplyDelete
  5. Kwanza alipataje hii permit ya kazi? Je alitimiza vigezo vya kupata ajira kama mtaalamu wa fani ambayo ni vigumu kumpata mzawa?

    ReplyDelete
  6. Waache waibiwe hao, ujinga wa kuajili raia wa kigeni utaisha lini Tanzania, inamaana hapo Iringa hakuna watu wazawa wa kuongoza hiyo kampuni, hilo ndo fundisho halafu mnasema zawadi nono itatolewa ili iweje, kwangu Zawadi NONO mpe kazi mtanzania azibe pengo

    ReplyDelete
  7. Hakuna haja ya kutandaza hati ya kusafiria na kibali chake. Kama vipi wekeni hadi mkataba wake wa ajira basi.
    Na hiyo zawadi nono ndio ipi?

    ReplyDelete
  8. Safi sana,kwani Tanzania hakuna mameneja mpaka mtuletee wahindi?

    ReplyDelete
  9. Jamani watanzania hawapoooooooooo
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  10. ...a managerial job for a foreigner? I don't get it!

    ReplyDelete
  11. Yuko kwao Pakistan sasa anafuta pasi nyengine kwa jina jingine apate kwenda Dubai kufungua duka maana mtaji ameshaupata Bongo. Alikuwa meneja wa nini mpaka ajiriwe maana kuna WaTz kibao wenye elimu za kutosha kuwa meneja wa tawi? Hiyo ndio faida ya kuajiri mgeni. Hiyo kama mnamtaka kweli mpeleke taarifa kwa Aga Khan maana wahindi huyo wanayemuamini kuwahukumu.

    ReplyDelete
  12. Ndio mkome siku nyingine kwani huwezi kuajiri mtanzania akawa meneja? Lishakukuta ndio unaanza eti nimeibiwa wakati umemfuata mwenyewe pakistani mpaka tanzania,mm simlaumu huyo jamaa,

    ReplyDelete
  13. Hii safi sana. Watanzania wapo mnaajiri Wapakistan!! Hivi anao ujuzi gani ambao usingepatikana nchini? Ama kwa vile dugu moja? Serves you right!!!

    ReplyDelete
  14. Mkome na kukoma, tamu chungu sasa, kazi ya umeneja mumempa mpakistani kwani MPINGO mtanzania halisi hawezi kazi hiyo? wapo wabongo kibao wangeweza fanya kazi safi tu,wapakistani njaa tupi, alau mmbongo utajua uanzie wapi kumtafuta, I don`t feel sorry for the company, next time hire mzaramo, mnyamwezi, mkinga, mngoni na kabila lolote la mzawa wa bongo, si unaona ulaya, kazi wanapena wenyewe kwanza, zikibaki ndo wanawapa raia wa nje.

    ReplyDelete
  15. Poleni sana ila si kuna WaTanzania wengi wazawa ambao wangepewa hizo kazi ambao wana elimi nzuri sana.au ni kwa sababu ni mwarabu?Tanzania ni muhimu kuamka na Serikali kuweka sheria nitakazowabana waajiri kama hawa.Nchi zingine kazi kama hizo za umeneja ni ngumu sana kumpa raia wa nchi zingine.Nasema hivyo kwa uzoefu wangu wa kuishi nchi nyingine hapa Duniani.Mtoto wa Kabwela,Sweden

    ReplyDelete
  16. Kama meneja wa iringa katoke nje, je huko headoffice dar es salaam wageni watakuwa wengi kiasi gani

    ReplyDelete
  17. safi sanaaa tena sana jamaa mbaguzi

    ReplyDelete
  18. Mbona wakati unamwajiri hukututangazia,

    ReplyDelete
  19. Waziri wa kazi ajiuzulu au tumtoweni kinguvu huko ofisini kwake watanzania wengi hawana kazi yeye anatoa vibari kwa wageni why? Au kwakua yeye hana njaa? Na huyo Moo atuachie tanzania yetu coz hatutakii mema wala kututhamini na ni aibu kubwa kwa TAIFA kumpa UBUNGE MTU KAMA MOO

    ReplyDelete
  20. Ni kweli kabisa uasia umezidi ndani ya kampuni hiyo. Acha wamwibie

    ReplyDelete
  21. Safi sanaaa mkome kuajiri Wagner wakati wazawa wanasota

    ReplyDelete
  22. Wizi hausiani na rangi au utaifa wa mtu, hivi hamjasikia taarifa za mijitu mijizi hapa Tanzania ambayo ni misomi na yenye hadhi kubwa kitaifa? Heshima ya taaluma sina haja ya kutaja angalau mfano mmoja lakini idadi yao ni kubwa sana.

    ReplyDelete
  23. Nina hon degree ya Logistics and Supply Chain Management na uzowefu wa miaka mitatu katika Logistics operation ninayoendelea nayo hapa UK, naongea Swahilina English kwa ufasaha.Kabila Mwafrica. Naomba kazi kwa Muajiri.

    ReplyDelete
  24. Huyu Mo ni mbunge alietarajiwa kuleta maendeleo kwa Watanzania!!!! hainabudi kuona lengo halisi la hawa wafanyabiashara kuvamia siasa

    ReplyDelete
  25. Hivi watanzania wangapi wanaibia waajiri kila siku. Nao wanaaminika. Acheni maneno ya kibaguzi. Tanzanians are not serious. Nina jirani zangu wanauza magari wahindi, as i am writing wako kazini wanafanya kazi saa hizi. Mtanzania gani utamweka saa hizi leo jumamosi. Pombe atakunywa saa ngapi.

    ReplyDelete
  26. Mtoto wa Kabwela,SwedenNovember 17, 2013

    Wewe anonymous unafikiri ungeenda India au Pakistani au nchi zingine wangekupa umeneja na ukiwa na ngozi nyeusi ndio hicho kitu hamna kabisa.Watanzania sio wote ambao hawako serious wengi tu wanashinda makazini na wanachapa kazi.Tanzania na nchi zingine za ovyo ovyo za Kiafrika imekuwa rahisi sana kuwaabudu wageni mnawapa ajira ambazo zingeweza kufanywa na wazawa.Wageni kama Wahindi n.k wanatajirika haraka sana na kuamishia utajiri kwao.Hao Wapakistani,Wabangladeshi,Wahindi n.k ni njaa tupu na wana dhiki tu kama sisi.
    Mtoto Wa Kabwela,Sweden

    ReplyDelete
  27. safi sana bora ameiba tu ila tatizo la sisi wabongo uvivu jamani ndo maana watu wa nje wanachukua nafasi za juu sisi tunabakia kufanya kazi mapokezi tubadilike ndugu zangu mlio nyumbani. Mdau London UK...

    ReplyDelete
  28. Kweli angeajiri watanzania sio wizi kabisa.

    ReplyDelete
  29. Mtanzania ni mvivu, awe Mtanzania Mhindi, au Mtanzania Mzawa. Nilishawahi kuwapa ajira wazawa kumi na moja katika biashara yangu. Mshahara mkubwa, usafiri, pensheni, matibabu bure na kadhalika. Lakini kila siku anaumwa, kila siku anaenda kuzika. Watanzania hawawezi hata mara moja kufanya kazi overtime, mpaka waende ulaya kubeba maboxi.

    Sasa siwezi hata siku moja kumwajiri Mtanzania katika kazi muhimu ya kampuni yangu. Hata hao wasomi sijui wanasoma nini chuoni, nilimwajiri msomi wa chuo kikuu Dar, hawezi hata kuandika barua kw akutumia MS word au power point presentation. Alinitia aibu sana wakati wageni walikuja katika kiwanda na alishindwa kuwaeleza kwa kiingereza fasaha jinsi tunavyosalisha katika kampuni. Sasa hivi, nina Wakenya tu na wanafanya kazi masaa 14 kwa siku, yule mwanachuo aligoma kufanya kazi night shift kuzalisha mali. Watanzania maneno sana lakini kazi hawawezi, siasa ya ujamaa na kujitegemea imeshaota mizizi.

    ReplyDelete
  30. Safi kabisa wewe unawaajiri Waparksitan ili uonekane wa maana kwa sababu ya rangi?waajiri watanzania wenzako kwa sababu ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKUMALIZAAA.

    ReplyDelete
  31. Watanzania bwana sio wote baadhi si wafanyakaai. Nimefanya kazi miaka 40. Umaarufu wangu ni mkorofi na mkali. Mimi ni Mama nilikuwa na watoto kama wengine lakini kazi ikizidi nalala ofisini naamka asubuhi nanawa uso naenda nyumbani kidogo kucheck kisha narudi kazini. Can a Tanzanian dare do that. Mimi nakwambieni nilikwenda hospitali India pale Apollo Hydrebad, wafanyakazi wa kawaida hawaendi nyumbani mpaka weekend, kwa sababu ya usafiri kwenda nyumbani na kurudi haiwezekani. Hivyo ukifika usiku pale reception utakuta watu wamelala. wanaamka saa 11 na kuanza kazi saa mbili. Ukichelewa kazini huna kazi. Mtanzania akichelewa kazini anaingia bila ya wasiwasi sababu ni usafiri na akifika anaanza hadithi ya kuelezea jinsi alivyotaabika kupata usafiri badala ya kuanza kazi, baadae anakwenda kunywa chai, ingawa kazi nyingi za serikali hamna lunch hour lakini watanzania wanajichukuliya one hour kwenda lunch serikali na katika mashirika ya Umma ukilalamika wewe ni mkorofi.

    ReplyDelete
  32. Inasikitisha kuona jinsi hii kampuni inavyobagua Watanzania katika swala la ajira kwa kuajiri wageni kwenye Nafasi zinazoweza kujazwa na wazawa. Huyu ndio Mohamedi watanzania waliyemuamini na kumpa ubunge? Inashangaza na kusikitisha! Acha wakuibie tu ujifunze kuamini watanzania. Uhamiaji sijui wanatoaje vibali vya kuishi na kufanya kazi hapa nchini kwa watu kama hawa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...