MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian, Baloziwa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikuluya Rais Seychelles.
Hafla ya kuwasilisha hati hizo, imefungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya nchi hizi mbili. Takriban kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 hatukuwahi kuwa na Balozi aliyewahi kuwasilisha Hati zaUtambulisho nchini Seychelles. Mh. Balozi alifuatana na Brig. Gen. E.V. Milinga, Mwambata Jeshi, Ubalozi wa Tanzania Nairobi
Katika hafla hiyo ,Mheshimiwa Balozi alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais James A. Michel, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika biashara, uwekezaji, mashirikiano ya anga usafiri wa majini, ulinzi na usalama.
Pia Mheshimiw Balozi Burian alipata fursa ya kuona na na mawaziri wafuatao na kufanya nao mazungumzo:-
(i) Mheshimiwa Prof. RolphPayet, WaziriwaMazingira naNishati
(ii) Mheshimiwa Christian Lionnet, Waziri wa Ardhi naNyumba
(iii) Mheshimiwa Pierre Laporte, Waziri waFedha
(iv) Mheshimiwa Dkt Patrick S. Herminie, Spikawa Bunge
(v) Bib iBenjamine Rose, KatibuMkuu, WizarayaUtalii naUtamaduni.
Ubaloziwa Tanzania Nchni Kenya pia unawakilisha nchi za Sudani, SudaniKusini, Somalia, Eritrea na Djibouti.
MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian, Baloziwa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikuluya Rais Seychelles.
Mh. Rais James Alix Michel wa Seychelles akiwa katika mazungumzo na MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Mazungumzo hayo yalilenga zaidi katika Mashirikiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.
Rais na Mawaziri "walioelemika" na wenye kujua hali na mazingira ya tropiki (WASIO NA UKWASI); sio wenye kuvaa masuti ya sufi na hariri yenye kuhitaji air-conditioners = gharama za mafuta nk = mzigo kwa walalahoi!
ReplyDeleteP.S. Michuzi: Usibane...la sivyo, nitazidi kuiweka!
masuti si ukoloni mtupu - cultural imperialism - Sijamuona Dr Shivji amevaa hayo masuti. Watanzania tuko bado mbali. Yale ma kaunda suti na mao yaliishia wapi?
ReplyDeleteNakuunga mkono hapo juu. Viongozi wetu badilikeni acheni kuwa wabinafsi sana, suti tu kila kona, uliza bei zake utachoka.
ReplyDelete