Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,wakati akitoa taarifa yake ya kuhusu kuvuliwa nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo (kushoto),kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo akizungumza.
Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo

Na Ripota wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

MBUNGE wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujitoa ndani ya chama hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho hivi karibuni. Amesema yeye atakuwa wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo,kama wanavyofikiria watu wengine.

Zitto ameyatoa maneno hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,wakati alikizungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa  Arusha,Samson Mwigamba.

Zitto amekana kabisa kuhusika na wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo.

"Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini haukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.

Zitto aliendelea kusema "Huenda leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama; "Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakaekuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama kuhitimisha jambo hili mimi sitoki ng'o kwenye chama hiki labda wanitoe wao," alisema Zitto.

Zitto alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu. "...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa nahujumu chama hiki naumia kwa kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama imara na kuwakomboa Watanzania.

"...Sisemi kama mimi sina makosa,kwani mimi ni binadamu na nimefanya mambo mengi kwa chama changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa.

ZIFUATAZO NI TAARIFA ZAO

TAARIFA YA MH. ZITTO KABWE
TAARIFA YA DKT. KITILA MKUMBO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. KAMA CHADEMA WANAWEZA KUVUNJA KATIBA YA CHAMA CHAO NI KIPI KITAWAZUIA WASIIVUNJE KATIBA YA NCHI? DEMOKRASIA IPI INAYOHUBIRIWA NA MBOWE, SLAA NA LISSU ILI HALI WAO NI MADIKTETA WANAOKIUKA KATIBA? NI MASWALI YANAYOTAKA MAJIBU.

    ReplyDelete
  2. MHH CHADEMA KWISHNEY !!!!!

    ReplyDelete
  3. Unajua, ukiwa na mkeo ndani na mkawa na tabia ya kuzungumza kwa taratibu hasa mnapotofautiana kimtazamo katika mambo fulani fulani ya kimaisha tu....ndoa yenu inaweza kuwa na nafasi ya kuruka vihunzi vingi na hatimaye itadumu bila shaka..... na kila mmoja wenu atajifunza taratibu kumuheshimu mwenzie kwavile kwa njia hiyo atajua ni kitu gani mwenzangu hapendezwi nacho na ni kitu kipi anapenda; na pia atajua ni nini afanye ili kuepusha migongano na tofauti zinazoweza kudhoofisha ustawi wa ndoa hiyo .... hayo yakifanyika kwa muda wa kutosha na kujengeka kuwa kama tabia ya wanandoa hao....hata jirani watajua kuwa "ndoa hii ina amani" - Yaani ingawa mnazo changamoto, kutofautiana wakati mwingine n.k.

    Lakini kama jambo dogo tu basi kelele mpaka jirani wanakosa usingizi.....ujue hapo mnawapa watu faida....na hii ndoa/nyumba haitasimama....itaanguka tu siku si nyingi!

    Utulivu katika kushughulikia matatizo, tofauti na migongano inayojitokeza katika ndoa, jamii, taasisi au hata vyama (viwe vya kufa na kuzikana - kama vipo, au vyama vya siasa - ila siyo vyama vya "sihasa").... hujenga umadhubuti, uimara na uthabiti katika kuendesha maisha ya vyombo vya jinsi hii....

    Lakini kama mmetofautiana kidogo tu (ambako huenda ikawa ni hisia tu zisizo sahihi) basi toka, wewe hufai, nenda kwenu, wewe msaliti, unatumiwa na ..... hamuwezi kufika popote!

    Hasara mtakazo zipata: Mtapoteza heshima ndani ya jamii; mtapoteza imani ya watu kwenu; hamtaaminika tena; mtajijulisha kuwa mko dhaifu kwenye "ku-handle" tofauti zenu na hivyo kukosa sifa ya kuaminiwa na watu katika mambo makubwa zaidi...

    Yaani kama hata mkeo amekushinda kumuongoza huko ndani kwenu sasa wewe utafaa kumuongoza nani....Taasisi inayoonyesha udhaifu namna hii nani ataiamini?

    Wakati watu wanatakiwa kutuliza akili, kutengeneza mikakati iliyoenda shule, kujipanga kuzikabili changamoto na misukosuko inayoweza kukipiga chombo katika safari....maana hii ni siasa siyo "sihasa" kama ingekuwa sihasa watu wasingetaka kufia madarakani.....kwanini mtu analia akipoteza jimbo au kiti cha udiwani (achilia mbali huo "urahisi").... hii ni siasa bwana!

    Huko Chadema tunasikia watu mnavuana nguo (madaraka) hadharani.....Je huo ndiyo wakati wa kuvuana nguo? wakati watanzania wanatafakari maamuzi gani wafanye hapo 2015, nani ataweza kubeba dhamana ya kuleta upinzani wa kweli (hata kama atashindwa tu uchaguzi) nyie mnavuana nguo mbele ya wananchi.....Huu ni udhaifu mkubwa!

    Ikiwa mambo yenu ya ndani ya chama mmeshindwa kuyamaliza kwa taratibu ili kuthibitisha mlivyo na busara ya kuzikabili changamoto za ndani ya chama....mnatakaje tuwaamini kwa dhamana kubwa ya Taifa hili la Tanganyika?

    Mnahitaji kuchukua hatua za haraka na za dharura sana ili kuondoa hii kasoro kubwa na mjifunze kuzikabili tofauti zenu ndani ya chama na kutatua migogoro yenu bila kuwafanya jirani wakose unsingizi....huku mkiwapa faida bure...

    Tuhakikishieni kuwa mko makini....lasivyo hata hao mlionao sasa mtazidi kuwavua nguo....maana ukishindwa kuishi na mkeo wa kwanza....uwezekano wa kuwa na ndoa zisizodumu baada ya hapo ni zidi ya 80% - ni mtazamo tu!

    ReplyDelete
  4. Zitto Mkali na anaongea kwa points sana. Uamuzi wa busara kubaki kwenye chama.naona huu wote wivu tu ni smart kuliko wengine halafu ni kijana.

    ReplyDelete
  5. Well spoken Zittho Kabwe we love you so much unatumikia nchi.Mi nashangaa hao wafanya biashara na walanguzi wakiingia Ikulu si watatuuza? wamekosea mahesabu na afadhari wamefanya hata tukiwa hatujasahau kasi yako ya kukagua vyama. mtu pekee ameweza kuvumilia ni mh Kikwete ameweza kuvumilia uwajibikaji anaweza kusemwa hadharani sasa hao jamaa wakifika ikulu wapipingwa si watatupiga risasi? usiogope zitto tuko nyuma yako I know you very well since our childhood.

    ReplyDelete
  6. chadema wasipoangalia na wakajirekebisha haraka wamekwisha kabisa

    ReplyDelete
  7. Chama cha madictator hicho. Zittho tuliza akili hata wakikuzingua naamini umemfanyia kazi nzuri mh Kikwete hawezi kukutupa kabisa atakukumbuka tuu hata kama uko upinzani kwani mh Raisi anajali kutumikia wananchi zaidi ndo maana anakupenda na waona vinyongo eti unatumiwa.

    ReplyDelete
  8. Mheshiwa Zitto hao wanaokushutumu waache waseme wanavyotaka kwa sababu wewe hutukani bungeni wala hufanyi fujo bungeni kama hao wenzio, sasa wao wanaona huko pamoja nao. Baba wewe mstarabu kutoka usitoke wewe Chadema damu watoka wenda wapi? Anonymous

    ReplyDelete
  9. Mh. Zitto, wewe kaza tu buti. Hawa wazee hawana uchungu na nchi km wanavyojifanyaga. Wanawaita wenzao mafisadi. Wao ni marududu na punguani kabisa.

    Kama mmetofautiana, wasomi km nyie mnashindwa kukaa mkajadiliana kwa utaratibu utakao faa. Yaani piga ua, siwapi tena kura Chadema ktk uchaguzi wa uraisi.

    Zitto kaza buti kijana. Tuko nyuma yako. This country has waited for a strong leader like you for too long. Please dont give up now.

    ReplyDelete
  10. JAMANI HUO NDIO MWISHO WA CHADEMA !! HATA IWEJE HATUTAWAAMINI TENA , SIDHANI KUTOKANA NA HILI HAKUNA HATA MTANZANIA YEYOYE ATAKUWA NA IMANI NA NYINYI TENA - AFADHALI MKIVUNJE CHAMA GAWANENI ZILIZOKUWEPO MLE KABLA HAMJAFA , KWANI MAISHA YENU YAMEFIKIA MWISHO KI UMRI . ZITTO BADO KIJANA NA NCHI INAMKUBALI KWA LOLOTE, KAJITOA MUHANGA KWA KUTAKA HAKI KWA WANANCHI KUFATILIA MPAKA PESA ZA MAFISADI HUKO USSWISS LAKINI BADO MNA MUONA MSALITI. BASI WEAACHIE HAO WACHAGA WAWE WAO VIONGOZI ILI WAWE NA CHAMA CHAO KAMA WATUSI WA RWANDA AMBAO HAWATAKI MCHANGANYIKO NA KABALA LINGINE .

    LAKINI CHADEMA MSISAHAU SASA KASI YENU IMEFIKIA UKINGONI.
    MNAJIFANYA DEMOKRASIA KUMBE HATA NYUMBA ZENU HAZINA HIO DEMOKRASI SASA MTATAWALA LINI NA UBAGUZI HUO?

    NA HIVI SASA JUENI KANA KWAMBA KUANZIA SASA WANACHAMA WENGI WENU HASA MKOA WA KIGOMA ,MBEYA NA SHINYANGA WOTE WANAWATOKA NDUKI SASA HIVI , NA WAO NDIO ILIKUWA INAKUPENI KURA NYINGI KATIKA MOVEMENT ZENU.

    SASA MTAULA WA CHUYA!

    ReplyDelete
  11. Mtangoja sana chadema ife. Mnadhani ni kama ccm mnanidhamu ya uoga?? Poor u maccm mmeshadadadia wakati yakweni yanawashinda. Milikuwa mnasubiri leo asemeanatoka cchadema ha ha haaa . Chadema na zito miaka kaki8. Mmepataje aubu sasa.
    Chadeema na

    ReplyDelete
  12. Zitto kinachomuongezea nguvu ni kujiamini.
    Na siku zote anayejiamini na kufanya mambo yake na akafanikiwa bila kuwashirikisha wakubwa zake au waliomtangulia.definately watachukia.
    Haya zitto yasikutishe.piga polish butt...ingia kambini lindo ulilinde...waondoke wao.

    ReplyDelete
  13. zitto funguwa chama chako tafadhali wacha hiki ni cham a acha wachaga please tunataka ufungue tutakufata

    ReplyDelete
  14. Dr Kitila, lie psychology of adolescence ulonifundisha UDSM iliniingia kwelikweli, Ashanti ila hiki unachofanya kwenye siasa bado sijakielewa vizuri, nahitaji Madera zaidi

    ReplyDelete
  15. Kama CHADEMA ni chama cha madikiteta si mumshauri Zito aende CCM tu.? nasikia CCM bado wanapokea watu wanaotoka upinzani...Au tatizo ni zaidi ya hilo?

    Najua pengine michuzi utaiminya hii pointi kwa sababu unazojua mwenyewe.

    ReplyDelete
  16. Anonymous wa mfano wa ndoa kwa kiasi upo sawa...labda nielezee mtazamo wangu kupitia maoni yako...
    Kama ni ndoa upo sawa kabisa. Ila hii sio ndoa.. ni taasisi ambayo wamiliki wake ni watanzania...mbowe..slaa..zitto na wengineo sio zaidi ya hiyo taasisi...hata mtei pia. Ila wanaweza kuwa na ushawishi lakini sio wamiliki..
    Katika taasisi yoyote ile kuna ya kuvumilika na yasiyo ya kuvumilika hata kama chama kitakufa....ni bora ufe kuliko kuishi kiunafiki na kijinga kwasababu unaogopa kufanya maamuzi...basi kwa mwendelezo huo hautakuwa tofauti na wengine waliopita au waliopo. Ni lazima tukubali kuwa na mwongozo...sasa kama mimi nikiona uongozi wa nchi haufai..kwa hiyo ni sawa kufanya njama za chini chini ili niupindue?? Ni bora nifuate taratibu zilizopo...bora nipitilize na kufanya makosa katika hizo taratibu kuliko kuwa muhaini...maana hata kama nilikuwa nania nzuri sitaeleweka.
    Katika hili chadema wapo sawa...kama ilivyokuwa sawa kwa ccm kumtimua kada wao maarufu zanzibar. Labda tuzungumzie katiba za vyama na sio chadema peke yake.
    Watanzania tukiweza kuwa open minded na kuacha ushabiki katika kila kitu tutaweza kuelewa vitu kiundani na kuwa na maamuzi ya busara na kuleta maendeleo katika taifa letu. Swali.... je ni sawa sisi kuendelea kuwa maskini wa kutupwa ilihali nchi yetu ina utajiri wote huu?? Nini kifanyike?? Na wasiwasi jibu lako litakuwa tuendelee kusikilizana katika ndoa.

    ReplyDelete
  17. Punguza UKUWADI kijana tatizo ulilewa sifa na sasa unaporomoka!
    Na kusema kweli ulikuwa 'GUNIA LA MISUMARI CHADEMA'RIP

    ReplyDelete
  18. RAIS MTARAJIWA ZITO NA HUKO IKULU UTARUHUSU MAWAZIRI WAKO WATATUE MATATIZO KWA KUTUMIA MITANDAO? KIONGOZI MAKINI NI YULE MWENYE TATIZO HULIWASILISHA KWENYE VIONGOZI WENZAKE NDANI YA TAASISI YAKE NA SI KUPITIA MAGAZETI NA MITANDAO, USICHUKULIE UJINGA WA WATANZANIA KUTOJUA KANUNI ZA UONGOZI KUWA NI USHINDI KWAKO. ZITO NA WENZAKO KAMA MLIKUWA NA NIA NJEMA KWANINI MLITUMIA MAJINA YA BANDIA YA KISHUSHUSHU?

    ReplyDelete
  19. Kazi kweli kweli, siasa hiyo, ukweli mnaujua wenyewe ila sisi watanzania ukweli tulioupata katika sakata hili ni kwamba wote nyie, Zitto, Chadema bado sana, hamjaiva, hamjui conflict resolution, hamna uvumilivu mna jazba zilizo mfanya Mrema kukosa uraisi miaka ileeee. Hamfai kutuongoza, mnafaa tu kuwa wabunge ili kuchochea kuvumgua uovu. Kwa sasa ni ngaz hiyo tu ndiyo inayo wafaa.

    CCM nao pia hawatufai,wana mabaya mengi (na mazuri pia wanayo) Ila mabaya yao hayavumiliki.Sijui 2015 tutamchagua nani jamani, mbona majangaaa.

    Wapi James Mbatia, jipange baba 2015 tukupigie kura.

    ReplyDelete
  20. Mmmmh nachanganyikiwa Zitto kaza Buti kama uko kwenyee HAKI mungu yuko upande wako .............. 2015 cjui KURA nimpee nani maana kila sehemu majanga MBATIA ntakupigia kura hawa wengine mmmmmmmmmhhhhhh MAJANGA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...