Millen Happiness Magese (kulia) akikagua baadhi ya miradi yake manispaa ya Mtwara.
 Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati.
Millen Happiness Magese akiwa amepozi na wanafunzi huku wakiwa wamekalia madawati aliyochangia katika shule hiyo.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mrembo huyo katika shule  ya Msingi Mjimwema.
Millen akizidi kukagua miradi hiyo leo.
Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiriamali hao wakati wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
Millen akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo madarasa yanajengwa na pia pia aliwanunulia wanafunzi hao madaftari kama waonekanavyo pichani.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu. Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi wilayani Mtwara.
Millen akipozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema nje ya darasa jipya linalojengwa na mrembo huyo.
Mbali na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa kipaumbele.
Mwanzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika manispaa ya Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kutoa ni moyo, kwa kweri millen umeonyesha uzalando wako kwa wa-Tanzania. that's is so sweet lady! mdau holland.

    ReplyDelete
  2. Sio mpaka useme uko wapi we toa maoni tu tutapenda... Nami namfagilia wawaaaa huyu mrembo

    ReplyDelete
  3. Dada Millen Happiness Magesa kazi unayofanya ni nzuri ambayo matanzania yoyote anatakiwa kuiunga mkono kwa sababu inabadilisha maisha ya watu. Hilo darasa moja halitii moyo uongozi huko uangalie jinsi ya kuweka mambo sawa. Nakushauri uchangishe hapo mkoani au Dar ukilenga kuungwa mkono kwanza na wakazi wa huko.Wanafunzi hao ambao ni madaktari na viogozi wa kesho pia wanahitaji kuendelea kufadhiliwa.

    ReplyDelete
  4. Hongera sn, uendeleze moyo huo. Najua ungeweza kuamua kununua gari hela Hy Na tusingekuhoji kwavipi unaongeza gari, lakini umeamua vzr kusaidia Na Wengine wajione wana haki ya kuishi vzr duniani

    ReplyDelete
  5. nami namfagilia wawaaaa huyu mrembo"

    ndio nini????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...