Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitafakari wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo Mhe. Dkt. Maalim alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Fulgence Kazaura akimtunuku Shahada ya Uzamivu (Ph.D) Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) katika Mahafali ya 43 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani tarehe 16 Novemba, 2013. Mhe. Dkt. Maalim alikuwa miongoni mwa Wahitimu 41 waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu siku hiyo.
Mhe. Dkt. Maalim na Wahitimu wengine wa Shahada ya Uzamivu wakiwa wenye nyuso za furaha.
Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Fulgence Kazaura (katikati mwenye joho jekundu) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Rwekaza Mukandala (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Wahadhiri wengine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...