Mkongwe wa muziki nchini Congo (DRC) Tabu Ley Rochereau (pichani akiwa amelazwa hospitali) amefariki dunia. Habari zinasema amefariki mapema leo asubuhi huko Ubelgiji alikokuwa amelazwa hospitali akiugua kiharusi.
Tabuley, aliyezaliwa November 13, 1940, alikuwa kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International na mmoja wa wasanii wakubwa katika bara la Afrika katika uimbaji na utunzi wa nyimbo.
Akiwa na mpiga gitaa hodari Dkt Nico Kasanda, Marehemu Tabu Ley alikuwa mwanzilishi wa mtindo wa Soukous, na kuufanya ukubalike kimataifa kwa kuchanganya midundo ya Cuba na Rhumba la Latin Amerika. Tumkumbuke kwa kibao chake "Mokolo Nakokufa"
Mwenyezi Mungu aipmzishe roho yako mahali pema peponi. Ameen
ReplyDeleteHii nyimbo sio ya salum Abdallah? Km yake ndiyo nani amekopi na kuppest ?
ReplyDeletemokolo nakokufa,siku nitayokufa, alikuwa akivuta hisia na kujiuliza iwapo kifa nchi kavu au majini, jinsi watu watavyolilia, atakumbuka na mikebe ya bia wakinywa mwisho wa mwezi, nk....
ReplyDeleteTumshukuru Mungu kwa Paskali Tabu, tujiulize nasi tutakumbukwa kwa lipi?
R.I.P Tabu Ley
ReplyDelete