Jeshi la Polisi
nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai
(DCI) Robert Manumba (pichani) amefikia umri wa kustaafu kisheria ambao ni miaka sitini (60) katika utendaji
wake wa kazi.
Aidha, katika
utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali
zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha
mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi
katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya
ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es
salaam (1987 – 1993).
Pia, amewahi
kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995
– 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu
wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu
ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa
msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 –
2006). Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa
makosa ya jinai nchini.
Aidha, Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza (DCI)
Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya
Jeshi la Polisi kwa weledi na uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi
ndani ya Jeshi la Polisi.
Pia, amemtaka
kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa namna yoyote
ile unaoweza kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama
ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
Hata hivyo,
wakati tataratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa upulelezi ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini CID makao
makuu, kamishina Isaya Mungulu, atakua
akikaimu nafasi hiyo.
Imetolewa
na:-
Advera Senso - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...