Naibu wazir wa Maji Mhandisi Benelith Mahenge (Mb) mnamo tarehe 12 Novemba hadi 16 Novemba 2013 alifanya ziara mkoani Dodoma na kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa kwenye wilaya za mkoa wa Dodoma na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Dodomaa -DUWASA.
Alasiri ya Jumamosi Novemba 16, alikutana na Viongozi wa Mkoa na Watendaji/wataalamu wanaosimamia Sekta ya maji mkoani Dodoma kwa ajili ya majumuisho ya ziara nzima. Mkutano huo wa Majumuisho ulifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Benelith Mahenge (katikati) akitoa maagizo juu ya miradi ya maji kwa wakurugenzi na Wahandisi wa Maji wa wilaya za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Naibu Waziri huyo aliyoifanya wiki zima alipotembelea miradi ya maji mkoa wa dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe. Jumanne Ngede.
Wadau na viongozi wnaosimamiasekta ya maji Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu waziri wa Maji akitoa majumuisho ya ziara aliyoifanya wiki zimakukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Dodoma.
Baadhi ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilayaza Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji (hayupo pichani) wakati wa majumuisho ya ziara aliyoifanyamkoani Dodoma kukagua maendeleo ya utekelezaji miradi ya maji. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mpwapwa Bi. Mwajina Lipinga, Mkurugenzi wa Bahi Bi. Rachel Chuwa na Mkurugenzi wa Kongwa Bi. Bibie Mnyamagoha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...