Meza kuu ya viongozi wa matawi ya CCM New York na DC wakimsikiliza msimamizi na msemaji mkuu wa mkutano huo bwana Isaac Kibodya. Mkutano wa CCM tawi la New York ulifanyika kwa mafanikio makubwa. Na hii ni mara ya kwanza kwa New York kuwa na tawi na kuweza kufanyika mkutano kama huu. Dhumuni la mkutano huo ni kuhamasisha Watanzania kujiunga na chama na kuchukua kadi hili mchakato wa kuchagua viongozi wapya watakao tambulika kichama na kiserikali.
Msimamizi wa mkutano huo Bwana Isaac Kibodya akizungumza, maneno muhimu ambayo bwana Kibodya alisisitiza katika mkutano huo ni kwanza ni mshikamano na umoja wa watanzania, pili ndiyo chama. Kwa sababu bila mshikamano kama watanzania hakuwezi kuwa na chama imara.
Katibu wamuda wa tawi Bwana Mseba akizungumza mbele ya wanachama katika mkutano huo. Bwana Mseba ndiyo mwimili mkubwa wa tawi la CCM New York.
Professor Lwiza Kamazima kati ya watu walikuwa bega kwa bega na Bwana Isaac Kibodya kufanikisha mkutano huo wa CCM kufanyika. Moyo wa kujitolea wa Profesa Lwiza ndiyo mafanikio ya kuwepo kwa mkutano huu kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la wasiyo lala NYC.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...