Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwafokea wafanyakazi wawili wa kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China baada ya kufumwa na msafara wake wakiiba mafuta ya Diesel kwenye tanki la lori la la kumwagilia maji (Boza) la kampuni hiyo tarehe 19 Novemba 2013 Katika kijiji cha Ntendo Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa alikemea tabia hiyo ya wafanyakazi wezi na kusema umekua ni ugonjwa wa mda mrefu unaozorotesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa.

Wafanyakazi hao waliokamatwa ni dereva William Ebron (kulia pichani)
na kibarua Isaya Godwin  ambao walifumwa majira ya saa nne asubuhi wakinyonya mafuta kwenye tanki la Lori hilo lenye namba za usajili T-518 BDV mali ya kampuni hiyo kwa kutumia mpira wa kupitishia maji na kumuwekea mteja kwenye dumu la lita tano, hata hivyo mteja huyo alifanikiwa kukimbia. Baada ya kuhojiwa walidai kuwa mteja wao huyo angelipia lita hizo tano kwa Tsh. 3500/= bei ambayo kihalali haiwezi kununua japo lita mbili za mafuta hayo katika soko. 
 Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ulikua ukielekea katika kata ya Mtowisa kwa ajili ya shughuli za kuhamasisha maendeleo ambapo ulikumbana na mkasa huo njiani katika Kijiji cha Ntendo. Barabara ya Sumbawanga - Namayere inajenga kwa kiwango cha lami na mkandarasi Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8 ambazo ni fedha za ndani.
Watuhumiwa William Ebron (kulia) na kibarua Isaya Godwin (kushoto) muda mfupi baada ya fumanizi wakiwa hawana cha kujitetea.
Mashuhuda wa tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mshahara mdogo, wana watoto na wazazi wanaowategemea. Sio kuwafokea bali kujua kwanini wanaiba na kuondosha hizo kero zao.

    ReplyDelete
  2. duh njaa zitatuua wabongo

    ReplyDelete
  3. siwatetei wezi wowote , lakini kuwadhalilisha hawa peke yake ni dhuluma, kuna majambazi( viongozi serikalini) ktk serikali yetu yenye kuchota mamilioni ya fedha mbona hamwafanyi kama mlivyowafanyia vijana hawa?

    ReplyDelete
  4. people steal to survive, our leaders are on state visits at $500+ per day, what a joke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...