MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) umevuka malengo ya ukusanyaji damu kwa asilimia 110 katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba 2013 ambapo jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka malengo ya chupa 35,000 zilizokuwa zikusanywe.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa Mpango wa Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda alisema Kanda iliyongoza kwa makusanyo ya damu ni Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Dodoma na Pwani ambako jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa, Kanda inayofuatia kwa ukusanyaji damu ni Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro,Arusha, Manyara, Tanga) iliyokusanya chupa 6,159.
Alisema katika kipindi cha mwezi oktoba 2012 hadi Septemba 2013 takwimu zinaonyesha chupa za damu 139,676 ambayo ni sawa na asilimia 99.8 ya lengo la kukusanya chupa 140,000 ilifikiwa hata hivyo Mpango wa Taifa wa damu salama unakusanya asilimia 26 ya mahitaji ya damu kwa mwaka.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...