![]() |
| Nape akihutubia wananchi wa Nyamongo, Tarime |
NYAMONGO, Tanzania
Matatizo yaliyokuwa yakiwakabili wananchi katika eneo linalouzunguka mgodi wa Barrick North Mara katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, yamepata tiba baada ya kikao cha siku nzima kilichofanywa juzi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye katika kijiji cha Nyamongo wilayani humo.
Nape alifanya kikao hicho lengo haa likiwa ni kuwasilikiliza wananchi wenye matatizo mbalimbali wilayani humo, kutimiza ahadi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Septemba mwaka huu baada ya kubaini uwepo wa matatizo makubwa yanayowakabili wananchi wa eneo hilo.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa wilaya ya Tarime, John Henjewele, Wakuu mbalimbali wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya hiyo, viongozi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na wawakilishi wa wananchi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...