Mhe Naibu Spika Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Masuala ya Jamii na Mazingira cha Umoja wa Mabunge ya Africa,Carribean na Pacific ambacho kinafanyika jijini Addis Ababa kama utangulizi wa Mkutano wa Mabunge ya nchi za ACP na Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Ulaya.Mhe Ndugai ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa mwaka wa pili sasa.Wengine pichani ni maafisa wa Sekretarieti ya Umoja huo.
Washiriki toka Tanzania wakimpongeza Mhe Naibu Spika Ndugai kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kumalizika kwa kikao.Pichani kulia ni Mhe Mussa Zungu,Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge na kulia ni Katibu wa Msafara huo Nd.Aggrey Nzowa ambae pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Maktaba Bungeni.Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...