mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto. Tuzo hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madaktari Waliosoma Vyuo Vikuu nchini (THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi NOVEMBA 23, mwaka huu, viongozi mbalimbai watapewa tuzo za kutambua

Kuhusu THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na Mkurugenzi  wa taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini wakiwa wengi, watahudumia watu wengi na jamii kubwa zaidi. Anasema, hadi sasa taasisi ina madaktari  wanachama zaidi ya 120 ambao wamesambaa nchi nzima. "Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha uboreshaji huduma za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma bora za afya kwa watanzania,"anaongeza. Madaktari hao ni wale walioamua kubaki nchini badalayakukimbilia nje
ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.

"Tuliamua kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri    zaidi kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu. "Dira ya taasisi yetu, tunaona watanzania wenye afya bora, huduma bora , na miundombinu bora katika kutoa huduma za afya nchini . Katika taasis yetu  nguvu yetu ni umoja;  wote ni sawa, kila mtu ni muhimu na kila mtu ni kiongozi.  Nguvu yetu ni matumaini,"anaongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...