Mafundi wa kampuni ya SMH/Rail ya nchini Malaysia wakiendelea na kazi ya kuunda upya moja wapo ya vichwa vya treni ambavyo vinaundwa kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi alitembelea karakana hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Vichwa hivyo ambapo wamemuahidi kichwa cha kwanza kitakabidhiwa kwa Serikali mwanzoni mwa mwezi Disemba 2013.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiongea na vibarua walioajiriwa na kampuni ya SMH/Rail kutoka nchini Malaysia, asubuhi alipofanya ziara kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro kuangalia maendeleo ya uundwaji upya wa Vichwa vya Treni vya Shirika la Reli Tanzania(TRL). Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuhakikisha kuwa vibarua hao wanapewa mikataba kama watafanya kazi zaidi ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyowataka.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akioyeshwa mpango kazi wa kampuni ya SMH/Rail na Mhandisi wa Kampuni hiyo, Eng. Mohd Hisham(Kulia kwa Naibu Waziri) ambayo inaunda upya vichwa vya treni katika karakana ya Reli Mkoani Morogoro. Naibu Waziri ametembelea karakana hiyo leo Asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni ambavyo viko kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa kwenye sekta ya Uchukuzi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi akiongea na Naibu Mtendaji Mkuu, Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Paschal Mafikiri (wa kwanza kushoto), wakati alipotembelea Karakana ya Reli Mkoani Morogoro, leo asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni. Kichwa cha kwanza kinategemea kukamilika mwanzoni mwa Mwezi wa Disemba 2013.
twende tu kwa mwendo wa kinyonga; hakuna sababu yeyote inayotuzuia kuwa na treni zinazotumia umeme na za kisasa. gesi iliyopo inatosha kuzalisha umeme wa kutosha. maji dar kila siku mafuriko; tungejenga mabwawa makubwa tungezalisha hata megawatt 5000 (megawatt elfu tano) na zaidi. lakini ndiyo fikra zetu finyu na ubinafsi na kuendelea kuwa manyapala wa wakoloni wetu
ReplyDeleteJamani matreni yashapitwa na wakati hayaaa, ala hivi Africa inamatatizo gani!!! asa nahii Tanzania, ina maana hawa viongozi hawatembei wakienda nchi zawenzao nao wakajifunza kwenda
ReplyDeletena wakati, matreni haya yameshapitwa kwa sasa, yaani nimechekaje eti wallipee wafanye matengezo, matengeno gani? kwa hiyo mikweche: Loh