Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
(kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo
mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya
Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi
ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO
Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA
ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre
Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Na.Mwandishi wetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba
Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na
hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.
Ombi
hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano
na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa
mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community
Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa
kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa
vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa
vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na
Visiwani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne
wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akifafanua
zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia
malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii
na zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
“Zaidi
ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa
karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka”
alisema Al-Amin.
Alitoa
mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake
umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na
ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.
‘Vipindi
mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii
vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa
mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...