Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe inaendelea kuunguruma, mashabiki wa Simba na Yanga katika maeneo mbalimbali Tanzania wanachuana vikali kuhakikisha timu zao zinaibuka na kitita cha shilingi milioni mia moja Taslimu!!..

Kilimanjaro Premium Lager inawakaribisha kushuhudia Bonanza kubwa la aina yake Jumapili hii tarehe 17 November 2013!, Mashabiki wa Simba na Yanga katika miji ya Tunduma na Morogoro watashindana katika michezo mbalimbali kama vile;
Foos Ball!!
Kuvutana kamba!!.
Soka la wachezaji saba kila upande aka “Seven aside” nk,
Nyama Choma na Burudani nyingine nyingi zitakuwepo…

Pale katika Mji wa Tunduma; Bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika uwanja wa Mwaka!!. Kutumbuiza jukwaani watakuwepo High Class Band…. aka Wazee wa Mjini!.

Na kule Mjini Morogoro – Mji Kasoro Bahari; Bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi “Kiwanja cha Ndege”!!. Jukwaani watatumbuiza…The Bikon Sound!.. aka Wazee wa Pamba!.

Bonanza za Kili Nani Mtani jembe Tunduma na Morogoro zitafanyika Jumapili hii tarehe 17 November!, kuanzia saa nne asubuhi, Hakuna kiingilio na wote mnakaribishwa!.

Je wewe ni shabiki wa Simba au Yanga???!!! Njoo usaidie timu yako kuibuka na mkwanja huu mnene wa Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...