Vimbwanga katika ukumbi wa Übersee-Museum mjini Bremen
Kikosi kazi cha The Ngoma Africa band a.k.a FFU Ughaibuni
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" a.k.a FFU watarajiwa kutumbuiza usiku wa Jumamosi Novemba 23, 2013 katika ukumbi wa Übersee-Museum mjini Bremen, nchini Ujerumani.
Wakazi wa jiji la Bremen na miji ya jirani watapata burani ya kung'oa na sululu kutoka kwa mzimu wa muziki Ngoma Africa band ambayo maarufu sana kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila wapandapo jukwaani.
Onyesho hilo limeandaliwa na makumbusho ya Oversee Museum ya jiji la Bremen kwa kushirikiana na Pan African Organization.
Ngoma Africa band wataanza kutumbuiza majira ya saa. 4.00 usiku na kabla ya hapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za kiafrika,pamoja na vyakula.
Bendi ya "Ngoma Africa " ambayo inadumu kwa muda wa miaka 20 imetajwa kuwa ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kufanikiwa kudumu katika medani ya muziki na kujizolea mamilioni ya washabiki katika kila kona duniani.
Watafiti wa mambo ya muziki wameitaja bendi hiyo kuwa inatumia kila nafasi waliyo nayo kuwanasa washabiki wake,na imetajwa mara nyingi kuwa ni bendi bora na kuchukuwa TUZO za kimataifa, ni bendi ambayo imepachikwa majina mengi mengi ya utani na kiusanii kama a.k.a "FFU Ughaibuni" ,aka "Watoto wa mbwa" chini ya uongozi wake Kamanda Ras Makunja wa FFU, Mtawala wa
himaya ya " Anunnaki Empire "
Usikose kuwasikiliza at
Watoto wa Mbwa,FFU naona ki-winter kimeshaanza nanyi bado mnaliendeleza gwaride,mbarikiwe amani ya bwana iwe nanyi
ReplyDeletekamanda mkuu ras makunja aka fiel-marshal namba 3 afrika,kwanza John Okelo, wa pili Idi Amin Dada na uliobakiwa wewe pekee , Kamanda nauliza hivi ? hamuogopagi baridi ! utauwa vijana baba,msimu wa baridi wewe ndio kwanza unaanza baraha.
ReplyDeleteKila la heri
Baba mtukutu kikamanda ketu ras makunja,mtawala wa himaya ya Anunnaki Elien a.k.a mkuu wa kikosi
ReplyDeletemahususi FFU ughaibuni,baba chonde chonde msimu wa baridi umeanza na wewe ndio kwanza unakaza buti