Tamasha la Filamu za Ulaya mwaka
2013 litaanza rasmi Ijumaa tarehe 22 kwa kuonyesha filamu
"Untouchables", kutoka Ufaransa katika ukumbi wa Alliance Française
saa mbili kamili usiku.
"Untouchables," filamu
iliyofanya vizuri kwa mauzo, iliyotayarishwa mwaka 2011, imewekwa katika
mandhari ya Paris na inahusu mabadiliko katika maisha ya msomi kutoka familia
inayoheshimika, pindi maisha yake yanapokutana na maisha ya Muafrika, ambaye
amemfata ili kumwekea sahihi katika nyaraka yake ya uhifadhi wa jamii (social
security) ili aweze kupata mafao yake.
Filamu hii imekuwa ikielezewa
kuwa ni filamu iliyochangamka, yenye kutia moyo na yenye mguso katika masuala
ya ulemavu na rangi lakini muhimu zaidi, ni filamu kuhusu urafiki.
"Tuna furaha sana kuwaletea
filamu hii nzuri katika ufunguzi kwa kupitia Tamasha la Filamu za Ulaya ambayo,
ingawa ina muonekano mwepesi, ni filamu inayoangalia hali halisi ya ulemavu na urafiki
wa watu wasiolingana," alisema Balozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Ceriani
Sebregondi.
Filamu 18 zitaonyeshwa mwaka huu
katika kumbi nne, Century Cinemax - Mlimani City , Nafasi Art Space, Goethe -
Institut na Alliance Française – zote bila kiingilio.
Waandaaji na waratibu wakiongelea kuhusu tamasha hilo la kila mwaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...