Mkalimani wa lugha ya Kichina , Dk Rashied  Kabongo ( kulia) akitoa tafsiri ya  lugha ya kichina kwa kishwahili kutoka kwa  Mkurugenzi Mkurugenzi wa Taasisi ya  Confucius ya China, Tong Jun ,wakati alipokuwa akitoa shukrani zake kwa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro na Serikali ya Mkoa mara baada ya uzinduzi wa mpango wa ufundishaji wa lugha ya kichina Chuoni hapo, tayari Taasisi hiyo inafundisha lugha hiyo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro, Profesa Hamza Njozi akitoa hotuba ya utangulizi.
 Baadhi ya wanachuo cha MUM.
 Wakisikiliza Hotuba.
  Mmoja wa wakufunzi wa Taasisi ya  Confucius ya China inayofundisha lugha ya kichina  hapa nchini , Wei Jianli ‘ Bi Shuxia’ ,akisikiliza moja ya swali kutoka kwa mwanafunzi mmoja wapo wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro akitaka kujua baadhi ya vitu vilivyopo mezani kwa maneno ya kichina ,  Nov 2, mwaka huu  baada ya uzinduzi wa mpango wa ufundishaji wa lugha ya kichina Chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi ( watano kushoto),katika picha ya pamoja na Viongozi wa MUM na Taasisi ya Confucius ya China inayofundisha lugha ya kichina Chuoni hapo.( Picha na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Profea samahani kama nitakukwaza. Mimi nilidhani hapo ndio tuonyeshe kiukweli kuwa sisi ni Muslim University, kwa hiyo hao ndugu zetu wa kichina tungewaazima tu mitandio wakajifunika vichwa halafu wakimaliza shughuli zao wavue. lakini kwa kukubali watoe mada wakiwa vichwa wazi mimi naona kuna mushkeli kidogo.

    ReplyDelete
  2. Hivi ninyi Waswahili Kiingereza hamjamaliza kusoma halafu mnaanza Kichina! Dah!

    ReplyDelete
  3. this is very nice Ni Hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...