Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Makamishna wawili wa Tume ya utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Walioapishwa katika hafla hiyo ni Dkt.Angelo Mtitu Mapunda na Mhe.Georgina Mulebya.Pichani Makishna hao Dkt.Angelo Mtitu M apunda na Mhe.Georgina Mulebya wakila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(picha na Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Novemba 6, 2013,  amewaapisha Makamishna wawili wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania.
Walioapishwa katika halfa hiyo iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam ni Dkt. Angelo Mtitu Mapunda na Ndugu Georgina P.K. Mulebya.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Jaji Mohammed Chande Othman, Jaji Kiongozi Mheshimiwa Fakhi Jundu, Majaji na watumishi wengine wa Mahakama.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

6 Novemba, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...