Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(Photos by Freddy Maro)
Kila la kheri Hon. JK katika huo mkutano na wakuu wenzio wa nchi za EA....tunaamini katika uwezo wako wa kushughulikia mambo ya ki-diplomasia na hivyo busara zako na uvumilivu ulionao vyote kwa pamoja vitaweza, kwa sehemu kubwa, kunusuru uhai wa EAC hata kama Jumuiya inapitia wakati mgumu kuliko wakati mwingine - angalau kwa kurejea mwenendo & matukio yanayoikumba EAC hivi karibuni
ReplyDeleteKumbuka kuwa hakuna President yeyote EA ambaye amefanya kazi kama Minister wa Foreign Affairs kwa muda mwingi kama wewe hivyo hii iwe chachu kwako kuwafundisha ma-raisi wenzio subira na uvumulivu unaotakiwa ikiwa kweli nao wanataka EAC iweze kuwa na haima njema....rest be assured, You have the support of our prayers - Tanzania kwanza, EA badaye!
Wadau hii imekaaje? Rais anapokewa na watu wa vyombo vya ulinzi na usalama? Kwa nini hapokewi na mwenyeji wake Rais M7? Jamani mbona hii inaleta ukakasi. Au ndio mbinu ya CoW kumuondolea mood Rais wa TZ kusudi asijenge hoja zenye tija wakati wa Mkutano. Mwanawane JK, we kuwa mpole. Kubali kuamua yaliyo na manufaa kwa TZ na kisha achana nao hao warafiki wasio waaminifu.
ReplyDeleteSpeech yako uliyoitoa bungeni mwezi uliopita, imewaweka sawa viongozi wa EAC. Hongera sana, usiogope kuongea ukweli baba yetu Kikwete. Mungu awe nawe daima. Nafurahi kama upo katika mahudhulio ya mkutano wa jumuiya hiyo.
ReplyDeleteOle wenu 'CoW' yaani Coalition of the Willing.
ReplyDeleteNi kuwa tayari Dakitari wa Mgonjwa Muungano wa (EAC-CoW) yeye Mhe. BALOZI DAKITARI BINGWA JAKAYA MRISHO KIKWETE ameshatua Kikaoni Kampala akiwa na SINDANO MKONONI TAYARI KUMDUNGA MGONJWA SINDANO YA MWISHO BAADA YA ILE YA KWANZA KUPITIA HOTUBA KUTOKEA BUNGENI DODOMA!!!
Tena imefaa sana ametua Entebbe na ''PRESEDENTTIAL JET'' ambayo ina vitu vitatu (3) ALAMA ambavyo Wananchi wapatao 130 Milioni Wakazi wa EAC wanazifahamu vizuri sana.
ReplyDeleteALAMA:
1.JINA LA TAIFA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''
2.ALAMA YA ABAM NA HAWA ''NEMBO YA TAIFA''
3.BENDERA YA TAIFA.
Kwa kuwa Mhe. BALOZI DAKITARI BINGWA Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE ni RAISI WA AFRIKA YA MASHARIKI KILA MWANANCHI KTK NCHI ZOTE 5 ZA UMOJA ANAWAJIBIKA KUZIFAHAMU ALAMA HIZO TATU (3) HAPO JUU!
Kuzifahamu Alama hizo 3 hapo juu ndio kama vile Hotuba alipoitoa Mhe.Raisi akiwa Bungeni Dodoma huku nchi zingine jirani (Majina kapuni) kuogopa hata kutoa Picha yenye Nembo ya Adam na hawa ktk Magazeti yao wakati Kikwete akihutubia!!!
Kwa Taarifa nilizopata wiki hii kutoka Kampala hadi Kikao cha jana cha Baraza la Mawaziri, NI WAZI NG'OMBE MWENYE MIGUU MITATU 'Coalition of the Willing' TAYARI AMESHA FARIKI DUNIA!
ReplyDelete''CoW'' tokea lini Ng'ombe akawa na miguu mitatu (3) ?'
Ingekuwa ni Miujiza, ndio maana wana Afrika Mashariki wengi nchi za nje na ndani walihoji sana Waganda na Wakenya walistaajabu sana kuona EAC isiyokuwa na Tanzania !
Tumezoea hadi umri huu tukijua na kuona ng'ombe akiwana miguu mine (4) na kichwa kimoja (1) kama hapo chini!
Yaani
MIGUU:
1.KENYA
2.UGANDA
3.RWANDA
4.BURUNDI
KICHWA:
1.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANANIA(BABA LAO MAKAO MAKUU NA MHIMILI WA UMOJA-Center of gravity where the destiny stays)
Mhe. Samwel Sitta amezungumza leo asubuihi ktk BBC ya kuwa sasa Maazimio YOTE MAKUU ''Protocols' yanasimamiwa na nchi zote 5 na sio 3 !
Ingekuwa ni maajabu ya Mussa ng'ombe mwenye miguu mitatu akaweza kuishi daima kama sio nG'OMBE KIGEGO AMA MZUKA, AMA NG'OMBE JINI ndio maana CoW hakuwa na maisha marefu tayari tikea jana amesha fariki dunia !
Mdau wa pili juu:
ReplyDeleteUnaonaje unapo pangiwa kukutana na Simba?
Ni wazi ni lazima utakwepa kupita njia ambayo utakutana na mnyama mkali, Kikwete ni DUME Na SIMBA MKALI ndiyo maana M-7 na kujifanya yeye askari amekwepa kuonana na Kikwete uso kwa uso!
M-7 kutompokea Kikwete haisaidii kitu!
ReplyDeleteMhe. Kikwete ni Jembe NI LAZIMA ATAWAPA VIPANDE VYAO TENA, kamwe hatawa kopesha kitu!
Hiyo ni mbinu ya Mbuni kuficha kichwa ktk rundo la mchanga wakati mwili mzima ukiwa nje !
Lo! kweli watanzania nawapenda, kwa kutoa maoni tu mnanifurahisha nafsi yangu. Hongera sana jamani
ReplyDelete