DSC_1899
Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji akibadilishana mawazo na aliyekuwa Rais wa Botswana Mh. Festus Gontebanye Mogae alipomtembelea rafiki yake Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) ofisini kwake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group Mh. Mohammed Dewji siku ya jana alipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake, aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae. 
Mh. Mogae ambaye pia amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya Mafanikio katika Uongozi itolewayo na mfanyabiashara mzawa wa Sudan Bwana Mo Ibrahim mwaka 2008, alikuwa na mazungumzo binafsi na Mohammed Dewji (Mo) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar-es-salaam.
Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, humuwezesha mshindi kupata kitita cha dola za Kimarekani millioni 5, na dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kwa maisha yake yote. Hizi ni baadhi ya picha, zilizopigwa na mpiga picha wetu  jana kwenye ofisi za MeTL Dar-es-salaam.
president (1)
Mh. Mohammed Dewji katika picha ya pamoja na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.
DSC_1903
Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji kwenye picha ya kumbukumbu na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...