Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (watatu kushoto) na baadhi ya viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa magugu na visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na vijana wajasiriamali katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,  alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari 500. Mbali na  kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa mchango wa kiasi cha shilingi milioni nne kwa ajili ya mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo yalitochukuliwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa vijijini.
Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
 Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha  pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hapo panapolimwa panafaa kulimwa kwa trekta.

    ReplyDelete
  2. Kinana na timu yako mnafanya very good job kwa sasa ila ningeomba itoke rohoni isiwe tu kuelekea 2015 na ushauri wa bure hata mngejigalagaza kwenye matope nadhani you have a long way to go kuwaridhisha watanzania na moja muhimu amabalo sikufichini ni jitihada za wazi za kuridhisha za kupambana na Rushwa otherwise yote yatakuwa diluted

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...