Mtaalamu wa michezo ya Karate na Yoga mtanzania Sensei Rumadha Fundi siku ya jumamosi November 16, 2013 Alitoa semina maalum ya mafunzo kuimarisha viungo kutumia vifaa asilia toka Okinawa "Chishi na jar" kuimarisha miguu, vidole na misuri yamapaja na miguu. Mafunzo haya yana lengo la kuimarisha nguvu za mateke na utumiaji wa ngumi, na kujenga msingi wa "Kata" bora.

Okinawa Goju Ryu Karate- Do "Special training for weight and conditioning" Sugarland, Texas, USA.

Sensei Rumadha Fundi (Black belt,3dan) ni mtaalamu wa mda mrefu katika michezo ya Karate ambaye alipata mafunzo ya mwanzo katika Dojo la Zanaki,jijini Dar-es-salam nchini ya mwalimu wake Marehem Sensei Nantambu Kamara Bomani. baadaye mafunzo ya Yoga nchini,Mafunzo ya juu na falsafa ya Goju Ryu kule Okinawa,Japan na kutunikiwa dan tatu.

Sensei Rumadha Fundi ni mmoja wa wataalamu wa kiafrika wachache wanaokubalika kimataifa katika fani hii Karate, Pia ameweza kuendesha mafunzo na semina katika nchi mbali mbali duniani. SENSEI RUMADHA FUNDI KUTOKA USWAHILI NI MTALAAMU WA KUJIVUNIA KWA WATANZANIA.

Sensei Rumadha Fundi (kaki) akitoa mafunzo ya nguvu kwa wanafunzi wake.
Sensei Rumadha Fundi akiendelea na yake.
Bi.Anita Mke wa Sensei Rumadha akimpa Pongezi Mumewe katikati kwa kumaliza kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Big up Rumadha....You make us proud....Always Vizuri kuona waTanzania tuna Excel. na your PERSONAL dedication na mafanikio -Hongera. "Big Will"

    ReplyDelete
  2. Hii ni sanaa yenye kuhitaji nidhamu upole katika maadilifu ya maisha na kulinda afya yako.
    Pia Karate inafunza juhudi na kuwa na ustamilivu katika maisha na kuitumia karate kama silaha ya kujilinda tu. Sio ugomvi kama vile baadhi ya watu wanavyo fikiria kuhusu hii sanaa, mbali ni mwenendo wa maisha.

    ReplyDelete
  3. Sensei Rumadha mototo mjini Kariakoo
    Hongera sana unatuwakilisha watoto wa mjini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...