Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} aliye kushoto akiongea na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah kabla ya shughuli ya kusaini Mikataba kuanza.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na Waziri mwenzake wa Kuwait wakisaini Mikataba ya Kukuza na Kulinda Vitega Uchumi; na Kushirikiana katika Masuala ya Utalii. Uwekaji saini huo ulifanyika nchini Kuwait siku ya Jumapili tarehe 17 Novemba, 2013.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na mwenzake wa Kuwait wakipongezana baada ya kukamilisha kazi ya kuweka saini Mikataba, Wanaopiga makofi ya furaha kutoka kushoto ni Mhe. Prof. Abdillah Omar, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ambaye anawakilisha pia Kuwait na Qatar na anayefuata ni Mhe. Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Membe akiongea na ujumbe wake, Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Uledi Mussa, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Gregory Teu, [Mb}, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye pia anashughulikia masuala ya Afro Arab, Mhe. Naimi Aziz na Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...