Sikubahatika kuonana nawe lakini hadithi zako lukuki nimezisikia, 
Kuhusu umahiri wako katika kinanda mpaka ukufunzi wako mashuleni.
Uongozi wilayani ulishika hatimaye kutinga Bungeni,
Hakika wanaIramba Magharibi wanakumbuka, sifa zako kwao kamwe hazikomi.

Familia yako uliiongoza, vijana wako wakakua wasomi,
Kama wewe ulisoma Ulaya, kwanini sisi tuishie njiani.
Hofu ya Mungu bado tumeishika, mafundisho ya Biblia hatuwezi acha,
Na mapambio tunazidi imba, tukijikumbusha kufundisha kwako kwaya.

Kwa kweli Babu ulisifika, kanuni za TANU ulizishika,
Taifa lako uliitetea, hansard zipo zinatuonyesha,
Uadilifu wako katika kazi tutaendeleza, busara zako tunazichota,
WanaIramba tutawatetea, kuhakikisha yale yote mazuri uliyoacha yanaendelea.

Kwa yakini sifa zako kidekede siwezi kumaliza zote, kwani uhondo uko mwingi,
Lakini hili la mashairi katu siwezi acha, maana kiburudishayo moyo ni la msingi.
Nabaki tu kujishangaa, haya vipi mjukuu nimeweza andika,
Hakika uandishi wako mwanana uliwavutia wengi, kama maji yafatavyo mkondo wake basi urithi wako siwezi kwepa. 

Tamati nimefika, sasa yatosha kusema,
Pumzika kwa amani mzee Yona, iko siku isiyo jina wanaIramba watashuhudia na pasina woga watanena, kwamba wewe kweli ni shujaa wangu nisiyemuona. 

Na Amani Geoffrey Nkurlu katika kumbukumbu ya 42 ya Hayati Mwalimu Yona Mazeynzile Nkurlu (Mbunge Iramba Magharibi 1965-1970)

-          06 Novemba 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...